Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 14, 2012

Rais Kikwete azindua blogu ya CCM Dodoma


Mwenyekiti waChama Cha Mapinduzi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua tovuti pamoja na Blogu ya CCM katika viwanja vya Ofisi kuu ya CCM Mkoani Dodoma jana jioni.Wapili kushoto ni katibu mwenezi wa CCM Nape Moses Nnauye, Watatu kushoto ni Makamu wa CCM bara Pius Msekwa, Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Bwana Wilson Mukama na viongozi wengine waandamizi wa Chama
 Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiangalia blogu hiyo mara baada ya kuizindua rasmi jana jioni mjini Dodoma.
Muonekano wa Blogu ya CCM iliyozinduliwa mjini Dodoma jana jioni
Muonekano wa Blogu ya CCM iliyozinduliwa mjini Dodoma jana jioni
Baadhi ya Wanachama wa CCM walihudhuria uzinduzi wa Blogu ya CCM uliofanyika mjini Dodoma jana jioni.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wanachama wa CCM waliohudhuria uzinduzi wa tovuti na blogu ya CCM katika viwanja vya makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana jioni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...