Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 9, 2012

WASHINDI ZAIDI WAIBUKA NA KUONDOKA NA JENEReTA NA BAJAJ


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager.
Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo (tatu kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia zake za Tusker Lager, Plisner Lager na Serengeti Lager, kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serebgeti (SBL) Teddy Mapunda,pamoja na Bw. Bakari Maggid kutoka shirika la Bahati Nasibu ya Taifa na kushoto ni muwakilishi kutoka kampuni ya PWC,Tumainiel Malisa
Meneja wa Bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungumza na mmoja wa washindi kwa njia ya simu 
Pichani ni Wawakilishi kutoka kampuni ya Pricewaterhouse Coopers (PWC),Tumainiel Malisa (shoto) na James Ndetiko (kulia) sambamba na  Bw. Bakari Maggid kutoka shirika la Bahati Nasibu ya Taifa wakifuatilia kupatikana kwa washindi wawili wa bahati nasibu ya Promosheni Vumbua Hazina chini ya Kizibo 

*****

Ni katika droo ya promosheni ya ‘vumbua hazina chini ya kizibo ’

Mei 9, 2012 Dar Es Salaam:  Droo ya pili ya  Promosheni inayoendelea ya kampuni ya bia ya Serengeti inayojulikana kama‘Vumbua hazina chini ya kizibo’ imefanyika leo katika ofisi za kampuni hiyo maeneo ya Oysterbay jijini Dar Es salaam.

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bidhaa zake, Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni nchi nzima ijulikanayo kama “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO.’ 

Promosheni hii ya aina yake iliyosheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta (kangavuke), Pikipiki, Bajaji, Gari ndogo aina (saloon) na zawadi zingine nyingi zikiwemo pesa taslimu. Katika promosheni hii zawadi za thamani zaidi ya Tsh MILLIONI 780 kushindaniwa.

Droo hiyo ilihudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers ili kuhakikisha washindi wote wanapatikana kihalali.

Akiongea waandishi wa habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni ya SBL Bi. Teddy Mapunda amesema kwamba  “Tayari tuna washindi zaidi ya elfu moja mia tano, wamejishindia pesa taslimu na kuzipata kupitia njia ya MPESA.  

Hawa washindi ni pamoja na wanaoshinda bidhaa zenyewe zilizoorodheshwa katika promosheni hii.  Vile vile,  kama mlivyoshuhudia asubuhi ya leo, tumepata washindi wawili wa jenerata, na sio mmoja kama ilivyo kawaida .  Hii ni kwa sababu katika promosheni hii, kuna vigezo na masharti yanayozingatiwa”.

 Masharti ya promosheni hii tunayazingatia kweli kweli na kwa  sababu hiyo, mshindi wetu wa wiki iliyopita  wa jenerata ilikuja kugundulika hakustahili kushiriki katika promosheni hii.  Tunataka kuwaeleza watanzania  kwamba hii promosheni ni ya uhakika na kwa kweli mnavyoona, ina uangalizi mkubwa na inaendeshwa kwa umakini kabisa.  Nawaomba wateja wetu waendelee kushiriki ili waendelee kushinda.” Aliongeza mkurugenzi huyo.

Washindi  katika droo ya leo waliojishindia jenereta ni Amadeus Minja mkazi wa pugu na Agnes Msengi wote wakia ni wakazi wa jijini Dar Es Salaam na Ibrahim Kimambo mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar Es Salaam aliyejishindia Pikipiki .   
Allan Peter Chonjo, Meneja wa Bia ya Serengeti Premium Lager alipiga simu kwa washindi na ilikuwa dhahiri kwamba washindi walishtuka na kufurahia ushindi wao.  Baada ya maongezi machache yaliyofanyika kwa njia ya simu washindi hao waliweza kujieleza vizuri majina yao kamili na wanapopatikana ili waweze kupatikana siku chache zijazo kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...