Akizungumza na
waandishi wa habari hao katika ufunguzi huo mkurugenzi wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa mchakato
wa shindano umefunguliwa rasmi ili kutoa fursa ya wadhamini kujitokeza kwa
wingi kudhamini shindano hilo ambalo litakuwa na mvuto wa aina yake kwa msimu
huu wa pili.
Pia wanamitindo
wenye sifa za kimataifa wameombwa kujitokeza kwa wingi katika usaili
utakaofanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada Apartments.
Tumeboresha
shindano kwa kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa hapo awali,lengo ni
kulifanya shndano hili liwe la heshima,hadhi na linalotimiza lengo lake la
kuvumbua na kuinua vipaji vya wanamitindo wa kchipikizi.
“Tunaomba wabunifu wadogo kwa wakubwa wajitokeze kuja
kuonyesha umahili wao katika shindano hili ambapo mwaka huu tutakutanisha
wabunifu wengi wa mavazi nchini Tanzania katika shindano moja kwa lengo la
kuwainua wabunifu wadogo na kuendelea kuwatangaza wabunifu wenye majina makubwa
katika tasnia ya mitindo hasa katika kipindi hiki maridhawa cha mwisho wa
mwaka” alisisitiza Magese.
Katika msimu huu wa pili wa unique model kutakuwa na
nyongeza ya mataji mengine madogo matatu amabayo ni “model photogenic
2012”,”model talent 2012” na “model with good manner 2012” ambapo mataji hayo
yatakuwa chini ya taji kuu la “Unique model of a year 2012”.
Fainali za shindano la Unique model 2012 zitafanyika
mwishoni mwa mwezi Desemba ambapo kamati ya maandalizi imedhamilia kufanya
onyesho lenye hadhi kuanzia ubora wa washiriki wenye vigezo vya uanamitindo ambao
wataleta mabadiliko katika tasnia ya mitindo nchini.
Shindano la Unique model lilianzishwa mwaka 2010
ambapo kwa mwaka huu ni mara ya pili kufanyika,Asia Dachi ndiye mwanamitindo
anaeshikilia taji hilo mpaka sasa.
Wito umetolewa kwa makampuni kujitokeza kuchukua
mabalozi ambao ni wanamitindo washiriki kwa lengo la kufanya nao kazi za
kutangaza bidhaa ama huduma inayotolewa na kampuni husika kwa lengo la kutoa
ajira kwa wanamitindo hao wanaochipukia katika tasnia.
Unique model 2012 imedhaminiwa na Dtv,Gazeti la
Tanzania Daima,Mashujaa investment ltd,Sophernner Investment co ltd,K.d.surelia,young
don records,Kiu investment ltd,Oriental bureau de change,100.5 Times fm,J’s
professional ltd,Lamada apartments hotel, na Unique entertainment blog.