Hali hiyo inadhihirika kwa kijana Ibrahim Class 'king Class
Mawe' ambaye anafanya vizuri katika medani za ngumi ambazo zinamsaidia
kuinua kiwango chake.
Tangu aingie katika mchezo huo ameshiriki katika mashindano mengi
na kufanya vizuri na kusababisha wadau mbalimbali wa masumbwi kumtabilia
kufika mbali mbali ikiwa atazingatia mazoezi.
King Class anasema alishawishika kuingia katika mchezo huo kutokana
na mapenzi aliyokuwa nayo tangu utotoni ambapo alikuwa na ndoto za kuwa
mwanamasumbwi.
Anasema kuwa ndoto yake ilianza kutimia baada ya kaka yake naye
anaeitwa Chaku Master kuwa mwanamasumbwi alikuwa akifanya vyema miaka
kadhaa iliyopita.
Chaku nilikuwa nikiishin naye hivyo wakati anakwenda kufanya
mazoezi nilimuomba kuongozana na hali iliyonifanya kuanza kucheza licha
ya kuwa ni ndoto yangu ya siku nyingi, anasema King Class.
Kocha wake wa kwanza kufundisha kucheza ngumi alikuwa ni mzee Babu
Tule ambaye alimpa misingi ambayo inamfanya hadi kuwa bondia mzuri
anaeshimu nidhamu na sheria za mchezo huo.
Mwaka mmoja baada ya kuwa na kocha huyo alimuamishia kwa
kocha Mkongwa Habibu Kinyogoli ambapo hapo alikutana na makocha wengi
akiwemo kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila
'Super D' ili kumpa mbinu zaidi za mchezo huo na kumjenga katika
misingi thabiti ya kufikia ndoto za kifikia mafanikio.
Anasema mwaka 2006 baada ya kuwa chini ya kocha wa siku nyingi
katika mchezo huo Kinyogoli kiwango chake kinakuwa kikiongezeka kila
siku na kuwa tishio katika ngumi za amacha.
Class anasema tangu wakati huo amepambana mapambano mengi ambao
alifanya vizuri na kumbukumbu yake inaonesha alifanikiwa kuwatwanga
wapinzani kwa KO katika mapambano zaidi ya 10, ndicho kitu anachojivunia
kwa sasa.
"Huwa najisikia faraja ninampompiga mtu kwa KO kwani inazidi
kunijengea heshima katika ngazi ya amacha ambayo ndiyo niliyopo kwa sasa
ambayo nahisi sina mpinzani," anasema Class.
Anasema siri kubwa ya kufanikiwa kufanya vizuri katika mapambano
yake ni kutokana na kuzingatia mazoezi, miiko, sheria na kanuni za
mchezo huo ambazo kila siku huwa anaelekezwa na kocha wa Kinyogoli.
Chipkizi huyo katika masumbwi anasema kila bondia anaweza
kufanya vizuri ikiwa atajihidi kusimama imara kuzingatia yanayokatazwa
katika mchezo huo.
"Moja ya vitu ambavyo avitakiwi ni uvutaji wa sigara na utumiaji wa
dawa kulevya ikiwemo Bangi na dawa nyingine ambazo ufanya kuwa na
uhamuzi usio sahihi," anasema Class.
Class anasema ikiwa bondia atatumia Sigara au akivuta bangi ufanisi
wake unakuwa mdogo kutokana na kifua kuwa kizito na kushindwa kumaliza
raundi za mchezo au anaweza kupigwa kwa KO.
Hivyo anawashauri mabondia ambao wanajihusisha utumiaji wa tumbaku
kuhachana na tabia hiyo ili kufikia malengo waliojiwekea katika
masumbwi.
Pia anasema unywaji wa pombe nayo ni sehemu inayonyong'onyesha
viungo, ikiwa bondia atahitaji kufanya vizuri ni vyema akaepiuka
utumiaji wa pombe.
Kingine anasema kuwa suala la uzinzi nalo ni tatizo kwa baadhi ya
wanasumbwi na ndiyo sababu kubwa inayowafanya kushindwa kufanya vyema
ulingoni na kuambulia kupigo kikali.
Hivyo anawaomba wanamasumbwi chipukizi na wakongwe kujiepusha na
hanasa hizo ambayo zinarudisha nyuma harakati za maendeleo ya mchezo huo
nchini.
Kijana huyo aliyemaliza taehe 10/10/1990 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya msingi Mafinga mwaka 2000, mkoani
Iringa anasema licha ya kujihusisha na masumbwi pia ni fundi wa vifaa
vya umeme ikiwemo pasi, TV, Friji,specer na vifaa vyote vinavyotumia umeme.
Anasema ili kuundeleza mchezo ni bora vifaa
vikatolewa kwenye klabu mbalimbali zinazoinua mchezo huu kwa vijana
wadogo ambao mara wamekuwa wakitatizwa na nyenzo za kufanyia mazoezi.
King
Class Mawe kwa sasa aliemia katika ngumi za kulipwa na kufanya vizuri
katika mapambano yake ya awali ikiwemo kumtwaga bondia Sako Mwaisege kwa
K,O ya raundi ya tatu na kufanikiwa kumdunda bondia mkongwe wa mchezo
huo Jonas Segu kwa point na kufanikiwa kuweka rekodi yake ya masumbwi
kuwa nzuriBondia huyo kwa sasa yupo kambini kwa ajili ya mpambano wake na bondia kutoka Tanga Said Mundi utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam
King Class Mawe kwa sasa yupo chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuakikisha kipaji chake kinakuwa na anapata michezo mbalimbali hapa nchini na matarajio yake ni kuwa bingwa wa Taifa na bingwa wa Dunia kupitia mchezo wa Masumbwi
--
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Mob;+255787 406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
No comments:
Post a Comment