Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya
kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika
mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini
Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada
ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 497
walijitokeza kushiriki mashindano hayo.
Mwanariatha Copro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza
mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano
yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’
yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi
1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na
kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City
Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/=
ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga
kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City
Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/=
ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga
kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City
Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/=
ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga
kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza
MWANZA, Tanzania
MWANARIADHA mahiri Copiro
Mwita wa Mwanza na Mary Naaly wa Arusha, jana waliibuka vinara upande wa
wanaume na wanawake, katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 ya ‘Rock City
Marathon 2012’ yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume akitumia saa
1:04:02, huku Mary akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa
1:16:33, katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wanariadha 497 waliokimbia
katika makundi matano.
Dotto Ikangaa kutoka Arusha aliibuka mshindi katika mbio za
kilometa tano wanaume, akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika
nafasi ya pili, huku Paul Elias kutota Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.
Rock City Marathon ni mbio zinazondaliwa na kampuni ya
Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa
na NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New
Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB).
Katika mbio hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa
na msanii maarufu wa Tanzania Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK
Wanaume, akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi
Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.
Rais wa Shirikisho cha Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka,
ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, licha ya kutoa onyo kwa wavamizi wa viwanja vya
michezo, alionesha kuridhishwa nuratibu wa Rock City Marathon, huku akiongeza
kuwa mbio hizi zimeweza kuibua vipaji vingi vya riadha ambayo vinahitaji
kukuzwa.
“Nawashukuru sana waandaaji wa Rock City Marathon kwa kuweza
kuandaa mashindano ambayo yameweza kutusaidia sisi wadau wa riadha kugundua
vipaji vingi ambavyo tunavyo hapa nchini ambavyo vinahitaji kukuzwa,” alisema
Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro.
“Hivyo basi natoa wito kwa makampuni, mashirika na hata
serikali, kuweza kudhamini mashindano kama haya ambayo yanasaidia sana
kuendeleza na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha ambao umeliletea sifa kubwa
taifa letu huko nyuma,” alisisitiza Mtaka.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alisema
Rock City Marathon imeonesha kuvuta hisia na kukubalika miongoni mwa washiriki,
kutokana na kuhusisha mbio za ngazi zote; nusu marathon, kilometa tano,
kilometa tatu kwa walemavu, kilometa tatu kwa wazee na kilometa mbili kwa
watoto.
Washiriki kutoka mikoa mbali mbali nchini walishiriki Rock
City Marathon 2012, pamoja na wageni kutoka nchi za India, Canada, Australia,
Afrika Kusini, Rwanda, Kenya na Uganda, ambapo washindi wa pili wa mbio za
kilometa 21, wanaume na wanawake walijishindia shilingi 900,000 kila
mmoja.
Washindi wa tatu kilometa 21 waliondoka na shilingi 700,000
kila mmoja na wa nne hadi wa 10 walizawadiwa shilingi 150,000 kila mmoja. Wale
walioshika nafasi ya 11 hadi 25 waliondoka na kifuta jasho cha shilingi 100,000
kila mmoja kwa upane wa wanaume na wanawake.
Jeremiah Kinshuzi wa Mwanza alishinda mbio za kilometa tatu
kwa wazee, huku Pascal Emanuel wa Kisese akishinda kwa watu wenye ulemavu na walizawadiwa
shilingi 50,000 kila mmoja, shilingi 30,000 kwa washindi wa pili na washindi wa
tatu wakijipatia shilingi 20,000.
Kwa upande wa watoto ambao walikimbia kilometa mbili, Idd
Suguta wa Mara na Emma Imhoff wa Singida waliibuka washindi na kuzawadiwa shilingi
30,000 kila mmoja, huku washindi wa pili wakipata shilingi 20,000 na wa tatu
15,000 na walioshika nafasi ya nne hadi
25 wakapata kifuta jasho cha shilingi 10,000 kila mmoja.
No comments:
Post a Comment