Mpambano
unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa ngumi nchini Tanzania na Ujerumani kati
ya Francis Cheka na Benjamin Simon wa Ujerumani sasa utafanyika tarehe 18
November katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani.
Awali
mpambano huo ulikuwa ufanyike tarehe 17 November jijini Berlin, Ujerumani na
tayari bondia Francis Cheka ameshasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa
Ujerumani anayejulikana kwa jina la “Iron
Ben” kwa ajili ya ukali wa makonde yanayowasulubu wapinzania wake.
Mtanzania Bondia Francis Cheka
Bondia
Benjamin Simon ana rekodi ya mapambano 24
ambapo amepoteza pambano moja wakati bondia Francis Cheka ana rekodi ya
mapambano 33 amepoteza mapambano 6.
Bondia Benjamin Simon wa Ujerumani
Akimwandikia
“Eva Rolle” wa kampuni ya “Primetime Event Management” ya
Ujerumani ambaye ndiye promoter wa mpambano huo, mwenyekiti wa ubingwa wa
IBF/USBA Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au
yeye mwenyewe Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa
watakaosimamia mpambano huo.
Hii
itakuwa mara ya kwanza kwa wababe hao kukutana kugombea mkanda wa IBF wa mabara
(IBF I/C) na mpambano wao unategemnea kutoa ushindani mkubwa.
Mshindi
katika mpambano huo ataingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora
kwenye uzito wa Super Middle duniani.
No comments:
Post a Comment