Onesmo Ngowi |
OCTOBA 22, 2012
Leo hii nilituma taarifa ambayo ilijaribu kuijibu makala iliyoandikwa na "Imani Makongoro" mwandishi mwandamizi wa gazeti la Mwananchi. Taarifa hiyo ya Makongoro iliyokuwa na kichwa cha habari “Umbumbumbu wa Imani Makongoro mwandishi wa gazeti la Mwananchi” ilitumwa kwenye vyombo vya habari leo hii!
Nataka kuchukua fursa hii kuifuta taarifa hiyo na kuwaomba radhi Imani Makongoro, gazeti la Mwananchi pamoja na wasomaji wote walioipata na kusumbuliwa na taarifa hiyo!
Nafanya hivi nikijua kuwa taarifa yenyewe ilitoka kabla ya kushauriana na washauri wangu. Naamini kuwa uandishi wa habari ni wito na unafanyika katika mazingira magumu sana hapa Tanzania.
Mimi sina nia ya kuisema wala kuikandamiza taaaluma ya uandishi wa habari. Aidha sina haja ya kuwafanya waandishi wa habari wasiandike yale wanayofikiri kuwa ni mema kwa jamii!
Ndiyo maana nachukua fursa hii kumuomba radhi Imani Makongoro, Gazeti la Mwananchi pamoja na wote waliopata taarifa ile kwa usumbufu walioupata.
SAMAHANINI SANA!!!
Imeandikwa na:
Onesmo Ngowi
Rais wa,TPBC, IBF AMEAPG, ECAPBA
Mkurugenzi CBC
No comments:
Post a Comment