Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo(kulia) na Jaji
,Joseph Migunda kutoka kampuni ya TAPBDS wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi
wa program ya Wezeshwa awamu ya pili iliyofanyika TBL Dar es SalaamMeneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo(kulia)
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa program
ya Safari Wezeshwa awamu ya pili iliyofanyika katika Ukumbi wa TBL Dar es
Salaam .Kushoto ni jaji wa program hiyo,Joseph Migunda kutoka kampuni ya
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi msimu wa pili wa programu
ya wajasiriamali ijulikanayo kama“Safari
Lager Wezeshwa”.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema kwamba programu hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha
wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na
ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili.
Bwana Shelukindo alisema, “Safari Lager kwa mara ya pili inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya
kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku
nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za
kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaoingia na kufuzu
vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni
kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika
kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua
kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio
wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini
kutoa hamasa kwa wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli
wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao.
Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa
watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali
kulingana na kazi anayofanya. Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwapa changamoto
wajasiriamali kujitahidi zaidi sio tu kwa ajili ya kujishindia ruzuku za
programu ya“Safari Lager Wezeshwa”
lakini kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla. Aliwasihi wajasiriamali na
wafanyabiashara kwa ujumla kutega sikio kwa taarifa zaidi juu ya usajili na
kutembelea website ya www.wezeshwa.co.tz.
Naye Bwana Joseph Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari Lager Wezeshwa”kutoka taasisi
ya TAPBDS, waratibu wa programu hiialisema kwamba sifa za kushiriki ni sawasawa
na ilivyokuwa msimu uliopita. Alieleza kwamba wajasiriamali watakaojitokeza
kushiriki wanapaswa kuwa na sifa kuu nne; wawe wachapakazi hodari, wawe wanamiliki
biashara binafsi ambazo ni halali, wawe na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na
wawe na nia ya kukuza biashara zao ili ziweze kuwasaidia wao na jamii
inayowazunguka. Bwana Migunda alieleza kwamba vigezo vinavyotumika kupata
watakaofaulu ni pamoja na kufuata vizuri maelekezo ya ushiriki, kuwa na wazo
ambalo ni la ubunifu zaidi, kuwa na biashara ambayo inasaidia jamii
inayoizunguka biashara hii nk. Alimaliza kwa kusema kwamba “Natoa wito kwa
wajasiriamali kote Tanzania wajiandae vizuri, watayarishe nakala sahihi za hati
za biashara zao, wasome na kujaza vizuri kwa usahihi fomu za ushiriki mara
zitakapotolewa na wawe na uhakika kabisa kwamba TAPBDS kama waratibu wa “Safari Lager Wezeshwa” tutahakikisha
vigezo vilivyowekwa vinatumika vizuri katika kumpata mshindi wa kweli”. Kama
ilivyokuwa mwaka jana, washindi msimu huu wa pili watawezeshwa kwa kupatiwa
elimu ya biashara na ruzuku za vitendeakazi mbalimbali kulingana na biashara
zao.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa
wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini mchango wao
mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa
wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia hii
inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha
wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia
kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
Mjasiliamali wa kutengeneza keki,
Elizabeth Chami (kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
baadhi ya bidhaa anazozalisha kutokana na mashine aliyowezeshwa awamu ya kwanza
wakati wa uzinduzi wa program hiyo awamu ya pili iliyofanyika TBL Dar es
Salam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mjasiliamali wa kutengeneza keki,
Elizabeth Chami (kulia)akimuonyesha Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo baadhi ya bidhaa anazozalisha kutokana na mashine aliyowezeshwa
awamu ya kwanza wakati wa uzinduzi wa program hiyo awamu ya pili iliyofanyika
TBL Dar es Salam.
No comments:
Post a Comment