Nembo ya Mbio za Rock City Marathon 2012, ikionesha wadhamini wa mbio hizo kwa mwaka huu.
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania, Dioniz Malinzi (wa tatu kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa wadhamini wa mbio za
Rock City Marathon 2012, wakifuatilia uzinduzi wa maandalizi ya mbio
hizo
uliofanyika kwenye Hoteli ya New Afrika. Rock City Marathon zitafanyika
Oktoba 28 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Oktoba 28.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jane Matinde
(kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 5, Meneja Matukio wa Kampuni ya
Capital Plus International ambaye pia ni Mratibu Rock City Marathon
2012, Grace Sanga jijini Dar es Salaam hivi karibuni kama sehemu udhamini wa
mbio hizo zitakazofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Oktoba 28
Oktoba. Airtel pia walikabidhi fulana 400 zitakazotumika katika mbio hizo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
JUMLA ya nchi tisa zinatarajiwa kushiriki katika mbio za
kilomita 21 za Rock City Marathon 2012, zilizoandaliwa na Kampuni ya Capital
Plus International (CPI), zitakazofanyika Jumamosi Oktoba 28 kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar
es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo Grace Sanga wa CPI, alizitaja
nchi hizo kuwa Kenya, Uganda, Rwanda,
Burundi, Jamhuri ya
Kidemokrasia Congo (DRC), Australia,
India, Canada na
Marekani, huku akidokeza maandalizi mazuri yamechangia ongezeo la washiriki.
“Tumetuma mialiko ya kushiriki kwa wadau wote wa riadha wa
nchi jirani ili wapate kushiriki Rock City Marathon 2012, ndio maana tunategemea
kupata washiriki wengi zaidi kutoka nje ya nchi, kulinganisha na mwaka uliopita
na maboresho ya mbio hizi yatachangia kuongeza ushindani,” alisema Grace.
Sanga aliongeza kuwa, mbio hizo za kila mwaka zimegawanywa
katika makundi matano ya mbio za kilomita 21 kwa wanawake na wanaume, kilomita
tano kwa watu wote, kilomita tatu kwa walemavu, kilomita tatu kwa wazee kuanzia
miaka 55 na kilomita mbili kwa watoto wa kati ya miaka saba hadi kumi.
Rock City Marathon zilianzishwa mwaka 2009, ambapo mwaka huu
ziko chini ya udhamini wa NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, Shirika la
Ndege Tanzania (ATCL), PPF, African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza
Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mbio hizo zinazosubiriwa kwa hamu na wakazi wa Kanda ya
Ziwa, zitapambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa nyota wa muziki wa kizazi
kipya nchini Juma Kassim ‘Sir Nature’, ambapo zitaanzia kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba kupitia njia tofauti na kurudi uwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment