Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 28, 2012

UMEWAHI KUMUONA ALIYETUNGA JINA LA TANZANIA? HUYU HAPA..



Mtunzi na Mwasisi wa Jina la Tanzania, Bw Mohamedi Igba (kushoto) akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi Abdulaziz Ahmeid mara baada ya uzinduzi wa msikiti wa madhehebu ya Ahmadiya mjini Lindi ambapo Igbar ndiye alikuwa mratibu mkuu na kufanikisha kukusanya Tsh 50Millioni. Mohamed Igbar aliasisi jina la Tanzania wakati akiwa mwanafunzi Tabora Secondary baada ya Serikali ya wakati huo baada ya muungano kutangaza kwenye magazeti kutaka wananchi wapendekeze jina na yeye kuibuka kidedea.
Kiongozi wa Ahmadiya  Nchini  Tahir Mohamedi,akitoa neno baada ya Uzinduzi wa msikiti huo
Waumini wa kiislam wa mjini Lindi wakishuhudia tukio hilo.
Waumini wa kiislam wa mjini Lindi wakishuhudia tukio hilo
Mssikiti uliozinduliwa unavyoonekana.
WATANZANIA wameaswa kujiepusha na vitendo vya vurugu, ili kuliepusha Taifa kuzalisha kizazi vitakavyoashiria udini na ukabila,hali itakayoweza kusababisha uvunjivu wa umoja, amani na mshikamano uliosisiwa na baba wa taifl Mwl Julius Kambarage Nyerere.

 Rai hiyo imetolewa jana na mwanzilishi wa jina la Taifa hili (Tanzania) Mohamedi Igbal Dar,alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari hizi muda mfupi baada ya kikao cha ndani cha
ufunguzi wa Misikiti uliojengwa mjini Lindi,kwa ufadhili wa Taasisi ya Ahmmady Iqbal, alisema vitendo vya vurugu vinayoanza kushamili hivi sasa hapa nchini, visipoangaliwa kwa umakini na kuchukuliwa hatua,vinaweza kulipeleka taifa kwenye machafuko yasiyoisha, na hivyo kuondoa sifa ya Tanzania aliyoiacha mwanzishi wa taifa hili, mwalimu Nyerere miaka kumi na tatu iliyopita.

Alisema kuwa vurugu zinazojitokeza hivi sasa kwenye Shughuli mbalimbali zikiwemo za dini pamoja na siasa, ni ishara mbaya kwa nchi kama ya Tanzania,ambayo imetimiza zaidi ya miaka  50 ya uhuru wake,na
kugeuzwa kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu.

Igbal ambaye kwa sasa maisha yake yapo nchini Uingereza, alisema kuna haja ya vitendo hivyo kudhibitiwa mapema iwezekanavyo kabla havijaota mizizi ya kuatarisha amani, umoja na mshikamano uliopo wa taifa hili.

Alisema kwamba vurugu sio jambo la kujivunia sana katika Taifa linahitaji kuendelea, kama la Tanzania  na kuwasisitiza  watu wasiojua athari za  kivita vya kidini  waangalie  nchi za  jirani  kama vile
Somalia  ambapo wananchi wake  wanaishi bila amani..

Nae kiongozi wa  Jumuia ya Ahmmadyya  nchini Tanzania Tahir Mohamedi, amewataka waislamu  kufuata  sheria  kanuni na makatazo ya mwenyezimungu  kupitia kwa Mtume wake Muhammad (Saw) kuungana  na kuwa kitu  kimoja  kwa kuwa dini yao,  haifundishi  waumini  wake kueneza chuki.

Tahir  alisema dini zote  dunia zinafundisha  amani, huruma na upendo miongoni mwa waumini wake watu wengine, lakini  ikiwa watu wachache wanaenda kinyume na  maagizo ya mungu  basi sio vizuri jamii
kuwahukumu waislamu wote wa Tanzania.

“Unajua  mwanzilishi wa Jumuhia ya waislamu  wa Ahmmadyya ametufundisha  kuwa ikiwa  mnapenda  kupata ridhaa ya mungu  basi takaseni  mioyo yenu  kwa kuwa  haina wazo la chuki  na fanyeni
uadilifu  hata kama  mbele yenu  kuna adui yenu” alisema Tahir

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...