Na Father Kidevu Blog, Tanga
Warembo
wawili wanao wania taji la Redds Miss Tanzania 2012, Happiness Rweyemamu (juu) na
Fina Revocatusi, (chini) usiku wa kuammkia leo wamechaguliwa kuwa Mabalozi wa Tanga
Beach Resort.
Mabalozi
hao walipatakina jana katika shindano dogo la kumsaka Balozi wa Hoteli hiyo ya
Kitalii ya jijini Tanga kwa warembo hao kupita mbele ya majaji.
Happiness
kutoka Kahama Shinyanga na akiwakilisha Kanda ya Ziwa ndie alishika nafasi ya
kwanza na kufuatiwa na Fina ambaye anatoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha na
anawakilisha Kanda ya Elimu ya Juujijini Dar es Salaam.
FINA REVOCATUS
Akitangaza
matokeo hayo Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndio waandaji wa
Miss Tanzania, Hasim Lundenga amesema mbali ya zawadi y ash laki nne kwa
mshindi wa kwanza na Laki mbili kwa mshindi wa pili lakini pia warembo hao
wamepata ajira Hotelini hapo.
Warembo
walio ingia tano bora ni pamoja na Brigitte Alfred wa Sinza, Happiness
Rweyemamu, Fina Revocatus, Diana Hussein na Balozi wa Naura Spring Hotel,
Eugene Fabian.
Warembo
hao wanao wania taji la Redds Miss Tanzania 2012 wamemalizia ziara yao ya
kutembeklea vivutia vya utalii Kanda ya Kaskazini jana katika mkoa wa Tanga kwa
kutembelea Mapango ya Kale ya Amboni.
No comments:
Post a Comment