Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing akizungumza
wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya gofu ya
NMB Nyerere Masters iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar
es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi wa SBL, Jaji
mstaafu Mark Bomani akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa
washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters iliyofanyika
katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing akimkabidhi zawadi mmjoa wa
washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Jimmy Mollel
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa benki ya NMB, Kees Verbeck akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters
Zawadi
Baadhi ya zawadi za washindi
Mshindi wa mashindano ya gofu ya NMB
Nyerere Masters, Abdalah Yusuph akivalishwa koti alilokabidhiwa kama
zawadi na Mwenyekiti wa Bodi wa SBL, Jaji mstaafu Mark Bomani katika
hafla iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam
Mshindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Abdalah Yusuph akiweka sawa koti lake alilokabidhiwa na Mwenyekiti
wa Bodi ya kampuni ya Bia ya Serengeti jaji mstaafu Mark Bomani baada
ya kuibuka mshindi katika mashindano ya NMB Nyerere Masters
Mshindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Abdalah Yusuph
akiwa na zawadi zake baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Mwenyekiti wa
Bodi ya kampuni ya Bia ya Serengeti jaji mstaafu Mark Bomani
(kulia) katika hafla ya kutoa zawadi iliyofanyika katika Viwanja vya
Gymkhana jijini Dar es Salaam
Washindi wa mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters wakiwa katika
picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na maofisa wa benki ya NMB ambao
ndio waliodhamini mashindano hayo ya kumbukumbu ya Mwalimu
Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Bia ya
Serengeti jaji mstaafu Mark Bomani (kulia) akimkabidhi mshindi wa
mashindano ya gofu ya NMB Nyerere Masters, Abdalah Yusuph (kushoto)
katika hafla ya kutoa zawadi iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana
jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi
wa Wateja Wakubwa wa benki ya NMB, Kees Verbeck na Ofisa Mtendaji Mkuu
wa NMB, Mark Wiessing (nyuma aliyenyoosha mkono)
Na Mwamdishi Maalum
Mchezaji
Abdalah Yusuph juzi aliweza kuwa mshindi wa mashindano ya ya golf ya NMB
Nyerere Master baada ya kushinda kwa mikwaju ya net 137 katika
mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Dsm gymkhana.
Mashindano
hayo yaliweza kushirikisha wachezaji zaidi ya 100 kutoka katika vilabu
vya Lugalo,Tpc,Moshi,Arusha gymkhana,Morogoro ,Kenya na wenyeji Dsm
gymkhana.
Kwa upande
wanawake mshindi alikuwa Young Suk Choi ambaye aliweza kushinda kwa
mikwaju ya netti 137 na nafasi ya pili ikaenda kwa Amina Khamisi
aliyepata netti 139.
Kwa upande wa
divion B mshindi alikuwa Vikasi Valma aliyeshinda kwa mikwaju ya netti
135,na nafasi ya pili ikaenda kwa Salumu iddy aliyepata netti 135
Katika
mashindano hayo ya NMB Nyerere Master kulikuwepo na mashindano ya golf
ya kulipwa ambapo Hassan Kadio aliweza kushinda kwa mikwaju ya gross
135.
Nafasi ya pili
ilikwenda kwa Yassini Salehe ambaye aliweza kupiga mikwaju ya gross
143,siku ya kwanza mchezaji huo aliweza kupata gross 69 siku ya pili
akapata gross 74.
Wachezaji
wengine Fadhiri Nkya aliweza kupata gross 146,Salimu Mwanyenza gross 149
Jeofery Leveriani gross 150 wote kutoka Dsm gymkhan.
Wengine John
Davids kutoka klabu ya Lessure [Mombasa] gross 153,Rajabu Iddi gross 157
Mbwana juma gross 157,Brayson Nyenza gross 164,Daudi Helela [Lugalo]
gross 164 na Salimu Dilunga gross 175 wote kutoka Dsm gymkhana.
Mashindano
hayo ya golf yaliandaliwa kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa mwalimu
julias Kambarage Nyerere aliyefariki miaka 13 iliyopita na yaliandaliwa
na chama cha mchezo wa golf nchini [Tgu] yakiwa chini ya udhamini wa
benki ya NMB
No comments:
Post a Comment