Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Stephen
Ulimboka pichani, leo ameeleza ya moyoni baada ya kutoa taarifa yake kwa vyombo vya
habari kupitia kwa wanasheria wake ambao ni Shayo na Nyaroro Kichere. Taarifa
hiyo imeeleza kuwa aliyekuwa anawasiliana nae kabla ya kutekwa, kupigwa,
kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye
kutupwa katika msitu wa Mabwepande usiku wa Juni 26 mwaka huu ni Bwana
Ramadhani Ighondu ambaye alidaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni Ofisa
wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Katika taarifa hiyo Dk. Ulimboka anaeleza
kushangazwa na kutokamatwa mtu huyo mpaka sasa na kudai kuwa yeye yupo tayari
kutoa ushirikiano kwa tume huru japo mpaka sasa haijaundwa.
|
No comments:
Post a Comment