Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel
Tanzania Beatrice Singano Mallya akihojiwa na vyombo vya habari katika
hafla ya uzinduzi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar
es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini
humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.
Waziri wa Viwanda na Maliasili wa
Seychelles, Peter Sinon (kushoto), wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania
Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia), mafundi na wawakilishi kutoka
Seychelees na Tanzania wakionyesha kipande cha mkongo wa mawasiliano
kama ishara ya uzinduzi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka
jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la
Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia
mradi huo.
Katibu Mkuu Idara ya Mwasiliano na
Teknolojia katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Seychelles, Benjamin Choppy
(katikati) akihojiwa na vyombo vya habari katika hafla ya uzinduzi wa
wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano
kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo
la Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia
mradi huo. Kushoto ni Mwakilishi wa kampuni ya Airtel nchini
Seychelles, Gail Talma Jumeau na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.
---
Waziri wa Maliasili na Viwanda wa
Shelisheli Bw. Peter Sinon amesema nchi yake itanufaika na upatikanaji
wa mawasiliano ya mkongo wa taifa kutoka Tanzania kwa ajili ya
kuharakisha maendeleo ya taifa hilo.
Mkongo wa taifa wa mawasiliano
uliozinduliwa miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya Kikwete umeweza
kuzinufaisha nchi jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na sasa
Shelisheli.
Akiongea katika fukwe za bahari ya hindi
jijini Dar es Salaam eneo la msasani ambako uwekaji wa mlongo huo ndio
ulikoanzia mwishoni mwa wiki hii Waziri Sinon amesema kuwa mpango huo
ukimalika utaiweza nchi yake kukuza sekta ya mawasiliano na upatikanaji
wa taarifa mbalimbali jambo litakalo saidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.
“Hii ni nafasi nzuri ya kipekee na ndio
maana hata sisi shelisheli tunaipa kipaumbele ili kukamilisha zoezi hili
la uwekaji wa mkongo huu wa mawasiliano, tunaamini tukimaliza kila kitu
itasaidia sana kukuza pato la nchi kulingana na umuhimu wa mawasiliano”
alisema Bw Peter Sinon- Waziri wa Maliasili na Viwanda Shelisheli
Kwa uapnde wake Katibu Mkuu kiongozi
kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw
Benjamin Choppy ameelezea faida za uwepo wa mkongo huo kuwa ni pamoja na
kutoa mawasiliano ya uhakika na bora kwa nchi hiyo
“Sasa hii ni dalili ya kutoa bidhaa bora
ya mawasiliano kwa kuwa ukamilifu wa uwekaji mkongo huu tutapata
mwasiliano bora zaidi” alimaliza kwa kusema Katibu Mkuu kiongozi kwenye
ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin
Choppy
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa
Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano Mallya ameelezea upatikanaji wa
teknolojia hiyo mpya ya mawasiliano kuwa ni kati ya vitu ambavyo Airtel
inavifanyia kazi kuhakikisha inaunganisha mataifa mengi ili kutoa
mawasiliano yanayotoa nafasi au fulsa ya kuendeleza nchi hizo kijamii na
kiuchumi pia
“Tunaamini ushirikiano wetu na wenzetu wa
shelisheli ni dhahiri utachangia sana kuboresha mahusiano yetu
kibiashara na pia kutoa nafasi kwa nchi hizi kujijenga kijamii ma
kiuchumu kutokana na faida ya mahusiano haya ya kulaza mkongo huu wa
kuunganisha mawasiliano” alisema Bi Beatrice Singano Mallya
Aitel Tanzania na Airtel Shelisheli kwa
kushirikiana na SCS zinatekeleza mpango wa kuweka mkongo wa taifa kwa
lengo la kuiwezesha nchi hiyo kuwa na mawasiliano ya uhakika.
No comments:
Post a Comment