Mkrugenzi wa kampuni ya LG kwa upande wa Tanzania akiongea na wageni
waalikwa waliofika katika uzinduzi wa Kinyoyozi kipya aina ya MULTI-V 3,
vinavyosambazwa na kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wakala pekee rasmi wa
kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG hapa Tanzania. Uzinduzi
huo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Msajili wa bodi ya wahandisi nchini engineer Steven Mlote akitoa
machache katika uzinduzi huo. Ambapo aliwashukuru kampuni ya LG kwa
kuleta teknolojia mpya ya viyoyozi aina ya MULTI-V 3 na vyenye ubora wa
uhakika.
Warembo wakifungua kwa taratibu pazia zilizokuwa zimefunika kiyoyozi huo ili kuashiria uzinduzi. |
Wakurugenzi wa kampunya LG na Wahandishi wa bodi ya Wahandisi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi. |
Umati wa watu uliokuwa umefurika kufuatilia uzinduzi huo.
Tanzania imechaguliwa kuwa moja kati ya nchi pekee chache barani Afrika
ambapo LG imeamua kuzindua viyoyozi aina ya MULTI-V 3, ambazo ni toleo
la tatu (tabaka la tatu) la aina ya viyoyozi aina ya VRF Air
Conditioning bora kwa matumizi ya majengo ya biashara na makazi ya saizi
ya kati.
Viyoyozi vya
Multi- V 3 vinafaida tatu kwa kuu kwa watumiaji ikiwemo ufanisiwa hali
ya juu, uwezo mkubwa zaidi na faida ya kuwa na bomba refu.
Kampuni la LG
linalenga kubuni na kukuza bidhaa zinazotumia nishati kwa ufanisi,
natamka kwa kujivuna kwamba bidhaa hii itakidhi matakwa bora ya wateja
pamoja usalama wa bidhaa kutokana na teknolojia ya udhibiti umeme na
zaidi kutokana na faida za utunzaji wa mazingira kwa viwango vya kisasa.
Alshaaf ndio
wakala pekee rasmi wa kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG
hapa Tanzania, naamini kwamba nchi yetu itaongoza katika kulinda viwango
vya kimataifa vya utunzaji wa tabaka la hewa na utunzaji mazingira.
Katika kipindi hiki cha mtikisiko wa upatikanaji nishati duniani, bidhaa
za LG zimeundwa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa zinazolinda
matumizi ya ziada ya nishati.
Tunawapongeza
washirika, LG na Alshaaf kwa jitihada zao endelevu za kutoa huduma za
ueledi za viyoyozi Tanzania kwa miaka 25 sasa na kujenga njia
inayoruhusu LG kuwa imara Tanzania kama wakala wao rasmi.
Alshaaf ni wakala pekee rasmi wa kusambaza na
kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG hapa Tanzania. Picha zote na Cathbert
Kajuna wa Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment