Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 13, 2012

KIKULA SPORTS BONANZA LAMALIZIKA KWA AMANI, HUKU TIMU ZA KITIVO CHA ELIMU CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) KUIBUKA WASHINDI KATIKA BAADHI YA MICHEZO ILIYOFANYIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA HAPO JANA


Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula Kisalimiana Na Wachezaji Wa Timu ya Mpira wa MIguu kutoka Kitivo Cha sayansi Ya Jamii kabla ya Mchezo wao Wa Fainali na Timu ya Kitivo Cha Elimu
Timu za Mpira wa Miguu Kutoka Vitivo Vya Sayansi ya Jamii na Kutoka Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa mbele ya jukwaa la mgeni rasmi Prof Idris Kikula Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)(Hayupo Pichani).Kutoka Kushoto Wenye Jezi za Blue Ni Timu kutoka Kitivo Cha Elimu na Mwenye Jezi za Orange ni timu ya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii Zote Kutoka UDOM
Mchezo wa Mpira Wa Miguu Ukiendelea Hadi Kufikia Mwisho Hakuna Aliyeona Nyavu Za Mwenzake na Ref kuamua timu zote kwenda kwenye matuta
Mchezaji wa Timu ya Kitivo Cha Elimu Edward Mzelu alipopiga Penati ya Mwisho Na Kuipa Ushindi wa Magoli 5 kwa 4 dhidi ya Timu ya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii na Kitivo Cha elimu Kuibuka Washindi wa Mashindano ya Kikula Sports Day Bonanza 
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula Akisalimiana na Wachezaji wa Mpira wa Kikapu Kabla ya MChezo huo Kuanza
Mechi kati ya Kitivo cha Elimu na Kitivo cha Sayansi ya Jamii ukiendelea na Kitio cha sayansi ya jamii kiibuka mshindi katika mechi hiyo
Mchezo wa Netball Kati ya Kitivo Cha Elimu Na Kitivo cha Sanaa na Lugha ukiendelea na Kitivo Cha Elimu kuibuka washindi
Tukibadilishana Mawazo na Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)Prof Idris Kikula (Wa pili Kulia), Wa Kwanza Kulia Ni Mmiliki na Mwandaaji Wa Mtandao Huu Wa Lukaza Blogu Bwana Josephat Lukaza, Wa Kwanza Kushoto Ni Kijana Abdul na Wa pili Kushoto Ni Mkuu wa Masomo ya Shahada ya Kwanza Prof Msofe tulipokutana Jana Katika Bonanza La Kikula Sports Day
Prof Idris Kikula (Katikati) akitabasamu wakati mchezo wa kukimbiza kuku kwa wafanyakazi ukiendelea katika bonanza lililofanyika jana Katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Msanii Chipukizi Chipoka akitoa burudani katika bonanza hilo lililofanyika jana katika Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Wadada waliojitokeza Kwenye Shindano la Kula katika bonanza hilo lililofanyika jana katika viwanja vya kitivo Cha Sayansi ya Jamii.
Zoezi la Ushindani Wa Kula likiendelea hapo
Washiriki wa Shindano la Kula Hao wakiendelea kushindana Kula katika Bonanza la Kikula Sports Day lililofanyika Jana katika Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma
Mshindi wa Shindano la Kula aliyeshikwa mkono akionyeshwa kuwa ndie mshindi wa kula katika bonanza hilo lililofanyika jana katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma ambapo lilidhaminiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idris Kikula pamoja na Kampuni ya Vinywaji Ya Coca Cola
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula alipokua akifungua bonanza hilo ambapo ilikua ni siku ya mwisho ya fainali ambapo karibia michezo yote ilikua ikikutana kwenye fainali.
Meneja Wa Kampuni Ya Coca Cola Kanda ya Kati Dodoma Bwana Maginga Akitoa Shukrani ka Uongozi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Na Vilevile Ndio KAmpuni iliyodhamini bonanza hilo Na Hapo alikua akikabidhi Zawadi Za Kreti za Soda kwa Uongozi Wa Chuo Kwaajili ya Kukabidhi kwa Washindi Wa Michezo Mbalimbali
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa bonanza la Kikula Sports Day likiendelea hapo jana katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu Cha Dodoma vilivyopo Katika Kitivo Cha Sayansi ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...