Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 8, 2012

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AZINDUA JUKWAA LA UCHUMI WA KIJANI MKOANI IRINGA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu Mkoani Iringa. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2012, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, Leo Mei 8, 2012, litakalofanyika kwa Siku tatu mkoani Iringa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, mkoani Iringa leo Mei 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Msanii wa Muziki wa Asili na Mashahiri, Mrisho Mpoto, akighani maneno yake yenye ujumbe Kuhusu Utunzaji wa Mazingira, mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliofanyika Mkoani Iringa leo Mei 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...