Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 10, 2012

RAIS OBAMA WA MAREKANI ASEMA NDOA ZA JINSIA MOJA ‘POA TU’.


Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kuunga mkono kuwepo kwa ndoa za jinsia mmoja na kuwa rais wa mwanzo kufanya hivyo.
Katika mahojiano yake na kituo cha luninga akiwa Ikulu ya Marekani, rais Obama ameeeleza kuwa alikuwa makini sana kuhusiana na suala hilo, kwani kwa watu wengi neno “ndoa” linamaanisha kitu ambacho kina hisia kali za kimila, kidini na kiimani.
Amesema sasa ni muhimu kwake “kujitokeza binafsi na kuthibitisha kwamba wapenzi wa jinsia moja waweze kufunga ndoa.”
BUSARA ZA MO BLOG: Viongozi na watawala wa Mataifa barani Afrika ikiwemo Afrika Mashariki na nyumbani Tanzania nini msimamo wenu kuhusiana na hilo..?? Kama mnapinga au kukubali wadau wanaomba sababu. Nanyi wadau wetu hapo je..?? Mnalakuongeza..??

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...