Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 7, 2012

SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA AWASILI KIGALI RWANDA KUHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA MASPIKA WA MABUNGE WANACHAMA WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kigali baada ya kupokelewa na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana (Kushoto). Mhe. Makinda yupo Kigali Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wananchama wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza na Mwenyeji wake Spika wa Bunge la Rwanda Mhe. Rose Mukantabana mara baada ya Kuwasili Mjini Kigali kuhudhuria Mkutano wa Saba wa Maspika wa Mabunge wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika leo. 

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipata maelezo  ya awali kuhusu Mkutano huo kutoka kwa maafisa wa Bunge la Tanzania. Wa kwanza Kushoto ni Bi. Justina Shauri , Afisa Dawati wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Bunge la Tanzania na Ndg. Charles Mloka, Mkurugenzi wa Kamati za Bunge anayemuwakilisha Katibu wa Bunge katika Mkutano huo. Picha na Owen Mwandumbya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...