Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 2, 2012

TUNAHITAJI UKUMBI BORA WA MCHEZO WA NGUMI

Mchezo wa ngumi  katika nchi yetu ya Tanzania unazidi kushika kasi
kutokana na kuchipuka kwa mabondia wengina mapromota ambao wanapigana
katika kuwania mataji mbalimbali nje na ndani ya Tanzania na 
kuandaa
mapambano . wapo mabondia wengi katika historia ya Tanzania ambao
wamewahi kupigana nje ya nchi hukiwauliza kuhusu ubora wa mchezo wa
ngumi katika upande wa vifaa vya mchezo huo ndani ya nchi yetu ni
imani yangu waliowengi wanaweza kukubaliana nami kuwa bado unahitaji
vitu muhimu ili kuendeleza mchezo huo .

Kwa Tanzania tumekuwa na mabondia wengi ambao wameweza kutingisha nje
ya Tanzania kama Joseph Marwa, Rashid Matumla,  Rogers mtagwa  na
Emanuel Mrundwa ambao waliweza kutwaa mataji mbalimbali ya mchezo huo
. jambo moja kuu ambalo watanzania tunalisahau ni kukosekana kwa kumbi
bora ya mchezo huo kwa upande mwingine kuna wakati baadhi ya watu
wanaohusika na mchezo wa ngumi waliwahi kuwa na wazo hilo lakini
nimeona jumatatu ya leo  nijaribu kulitilia mkazo .natoa mfano kama
tulivyo weza kujenga uwanja wa taifa na kuziona nchi kubwa duniani
zikija kucheza mechi za kirafiki kama Brazil basi hata mchezo wa ngumi
linawezekana ukitazama kama marekani ambao mchezo huu umekuwa kwa
kiwango cha juu kutokana nchi hiyo kuboresha maeneo ya kuchezea
kumbuka silinganishi kiwango cha mchezo bali ni namna ya
kuboresha.

Kwa Tanzania vipo vyama vingi vya mchezo wa ngumi PST,TPBC,TPBO bila
kusahau kile cha taifa cha BFT  lakini ni mara kadhaa Makore Mashaga
katibu mkuu wa BFT amekuwa akizungumzia juu ya ukosefu wa vifaa maeneo
ya mazoezi na kumbi za kupigania vimekuwa ni vikwazo vikubwa kwa
mchezo huo kwa Tanzania kwakuwa serikali imeweza kuleta uwanja mpya wa
mpira wa miguu ambao hata Suleiman nyambui anafaidika nao alikadharika
wanamuziki kupata studio ya kisasa ya kurekodia muziki  bila shaka
mchezo wa ngumi nao unahitaji eneo zuri la kuchezea mchezo huo kama
ilivyo Las Vegas Nevada na MGM Grand au Madson square ni dhahiri
inawezakana  kwa Tanzania kuwa na kumbi bora ya kisasa na imani vyama
vya mchezo wa ngumi vyote nchini vinaweza kukaa chini na kujadiliana
na serikali kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo kuhakikisha
tunapata kumbi bora ya kisasa ya kupigania  ili kuongezea ujuzi na
viwango vya mchezo wa ngumi kwa Tanzania.

kama ufilipino imeweza kutoa bingwa wa dunia hata Tanzania inaweza pia
kwani ukiacha soka mchezo wa ngumi ndio mchezo pekee ambao unakuja kwa
kasi pengine liwe ombi rasmi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania ambaye mwaka jana alitunikiwa tuzo ya heshima ya mwanamichezo
na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA kuwa
kiongozi bora kwa kujari michezo si vibaya Mh Jakaya Kikwete
akatuachia wapenzi wa masumbwi  kumbi bora w hata mabondia wanje
wajekupambana Tanzania kama zinavyokuja timu kubwa za mpira dunia
kucheza uwanja wa taifa .

nina maliza kwa kusema kuwa ni imani yangu kuwa kwa kujengwa uwanja
huo kutawapa mabondia wa tanzania kujiaamini  na kuupanua
mchezo huo
na unaweza pia kulitangaza jina la Tanzania  katika Nyanja za utalii
ndani na nje ya Tanzania kama inavyowezekana kuleta mastaa wa wakubwa
wa muziki kutoka ulaya na amerika ni dhahiri hakuna lisilowekana kwa
Tanzania .






No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...