Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 16, 2012

Washindi wa Kili Talent search wafikia 12


Washindi kutoka Dodoma kutoka kushoto ni Halima Ramadhani, Juma Madaraka na Issa Dubat
Kutoka kushoto ni Proffesor Jay, Henry Mdimu, Queen Darleen na Juma Nature.
 
Na Mwandishi Wetu
Washindi wa msako wavipaji unaodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, wiki hii umefikia hatua ya nne ambapo umefanikisha kupata washindi 12 ambao wamepata nafasi ya kurekodi nyimbo zao tayari kwa kuanza safari yao ya kisanii kupitia muziki.
Kwa mujibu wa waratibu wa zoezi hilo kampuni ya Frontline Novelli, tayari usaili umeshapita katika jumla ya mikoa minne na kila mkoa walikuwa wakichukuliwa washindi watatu watatu.
Akiifafanua zaidi kuhusiana na mchakato huo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Frontline, Irene Kiwia alisema washindi hawa watatu wa kila mkoa mara wanapopatikana hupewa nafasi ya kurekodi wimbo, kila mmoja na kisha kufanya wimbo wa pamoja wakishirikiana wote watatu.
Baada ya kurekodi washindi hawa watatu wote wanashiriki katika tamasha la washindi la mkoa huo ambapo kati yao mmoja atakayefanya vema jukwaani ndio anapata nafasi ya kushiriki tamasha kubwa la washindi litakalofanyi9ka mapema mwisho wa mwezi huu jijini dar es salaam.
Mikoa ambayo imeshatembelewa mpaka sasa ni Dodoma, Mwanza, Moshi na Mbeya ambapo washindi wake tayari wamesharekodi na katika mikoa ya Dodoma, Moshi na Mwanza, washiriki wa tamasha kubwa kabisa litakalofanyika mkoani Dar es salaam wameshapatikana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...