Makabu (kulia) na Gogito (kushoto)
Yale
mapambano mawili ambayo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu kubwa sana
katika bara la Afrika yamefanyika katika majiji mawili ya Johennsburg,
Afrika ya Kusini na Tunis, Tunisia baada ya kuibuka miamba miwili katima
ubingwa na uzito tofauti!
Katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Mkongo man Ilunga Makabu alimchakaza bila huruma bondia Gogito Gorgiladze kutoka nchini Georgia kwa TKO katika raundi ya nne (4)!
Mawili
hao walikuwa wanagombea ubingwa wa dunia wa vijana walio chini ya miaka
25 katika uzito wa Cruiserweight na mpambano huo ulirushwa moja kwa
moja na televisheni ya Super Sport!
Mambo
yalianza kujionyesha katika raundi ya kwanza tu wakati bondia Makabu
alipokuwa anarusha ngumi ya mkono wa kushoto ambayo ilikuwa inafanya
madhara yasiyojificha kwa Gogito!
Katika
raundi ya pili na ya tatu Gogito alikuwa anarudi nyuma na kuongea kana
kwamba anamwambia Illunga asimwadhiri mbele ya watu lakini Mkongo man
Makabu alisonga mbele akirusha makonde mazito bila huruma. Ilipoanza
raundi ya nne (4) Ilunga alirusha makonde sita ya kasi ambayo yalimfanya
referee wa mpambano huo Wally Snowball wa Afrika ya Kusini kuingialia
kati na kusimamisha mpambano huo!
Golden
Gloves ya Rodney Berman ndiyo iliyoandaa mpambano huo na Illunga
amepangwa kuteta taji lake mwezi ujao nchini Monaco katika tamasha la
“The Last Man Standing” litakalofanyika katika jiji la Monte Carlo!
Nchini Tunisia, bondia
anyeishi nchini Belgium, Ayoub Nefzi aliidhihirishai nchi ya Tunisia
kuwa yeye ndiye mtu pekee atakayeipeleka katika nafasi nzuri ya ngumi
duniani baada ya kumchakaza vibaya bondia Ishmael Tetteh wa Ghana katika
raundi ya 7.
Mpambano
huo uliofanyika katika jiji la Tunis uliwavutia mashabili wengi wa
nguni kutoka katika nchi za Afrika ya Magharibi na Kaskazini ambao
walifurika jijini Tunis kuuangalia.
Mpambano
huo ulikuwa wa kugombea ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya
Uajemi na Mashariki ya kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Jr. Middle na
uliandaliwa na Halmashauri ya jiji la Tunis katika juhudi zake za kukuza
'Utalii wa Michezo" (Sports Tourism).
Ayoub
Nefzi atakuwa kwenye kindumbwendubwe kingine nchini Belgium mwezi wa
tatu (March) kugombea mkanda wa juu wa IBF wa mabara (IBF
Intercontinental Title) hivyo mpambano wake na Ishmael Tetteh ulikuwa
kama wa maandalizi wake.
Hii
ni mara ya kwanza kwa IBF kufanya shughuli zake katika nchi ya Tunisia
kutokana na nchi hiyo kuegemea katika mashirikisho mengine ya ngumi!
IBF sasa inachukua nafasi ya katikati katika ngumi barani Afrika na hii inaleta hamasa kubwa kwa mashabiki wengi wa ngumi!
No comments:
Post a Comment