Yusuphed Mhandeni kulia akikabidhi viti kwa wana Yanga.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MCHUMI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Makumbusho,
Yusuph Shaban (Mhandeni), ameendelea kuwa kwenye Ilani ya chama chake kwa
kuwasaidia viti 10 vijana walioanzisha tawi la Yanga, linalojulikana kama Green
Stone, lenye maskani yake Mwananyamala Mwinjuma, jijini Dar es Salaam, karibu na ofisi za CCM.
Asante sana mdau wa michezo.
Kupeleka viti hivyo ni sehemu ya kuwaunganisha vijana zaidi
katika suala zima la michezo, huku wakiamua kuanzisha tawi hilo kwa ajili ya
kubadilishana mawazo pamoja na kuwa na mipango kabambe ya kujiletea maendeleo
siku za usoni.
Akizungumza jana katika makabidhiano hayo,
Shaban maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), alisema kuwa ameamua kutoa viti hivyo
kwa ajili ya kuwasaidia na kuungana mkono wanamichezo walioamua kujiunganisha
kwa kupitia klabu yao ya Yanga.
“Nashukuru kwa kufanikisha suala zima la viti hivi, ambapo
naamini nitakuwa karibu zaidi na wanamichezo hawa bila kuangalia wanatokea
katika timu gani,” alisema Yusuphed.
Naye Mwenyekiti wa tawi hilo la Green Stone,
Lomole Matovolwa, maarufu kama (Big) anayevuma pia katika tasnia ya filamu,
alisema kitendo cha Yusuphed kuwaunga mkono kinawafanya waamini kuwa tawi lao
litakuwa imara na lenye mipango ya aina yake.
“Hapo baadaye tawi letu litafanya mambo mengi ya
kimaendeleo ikiwamo wanachama wake wanaotoka hapa kufanya biashara, huku
tukiamini kuwa wadau tutakuwa nao sambamba,” alisema.
No comments:
Post a Comment