Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla(Pichani katikati) amesema itajumuisha vijana walioingia kumi bora, akiwamo Menina Atick, Nsami
Nkwabi, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na
mshindi wa milioni hamsini, Walter Chillambo.
Mshiriki wa shindano la Epiq BSS, Nsami
Nkwabi, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari,
anayetazama kushoto ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, Awaichi
Mawalla
Mshiriki mwingine, Norman Severino naye akiongea mbele ya waandishi wa habari
Katika
ziara hiyo pia, ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa
mashindano hayo mwaka 2006, wapenzi wa muziki watapata fursa ya kumshuhudia
mshindi wa Epiq BSS, Walter Chillambo ambaye atakuwa akizundua wimbo wake siku
hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Afisa biashara mkuu wa Zantel, Sajid
Khan, alisema dhumuni kubwa la ziara hiyo ni kuwajengea vijana hao msingi
katika kazi yao ya muziki baada ya shindano la Epiq BSS kuisha.
‘Lengo letu kuu la kudhamini Epiq BSS haikuwa
kumpa mshindi zawadi, la hasha, bali tulikuwa na mpango madhubuti wa kubadilisha
maisha ya vijana hawa kupitia vipaji vyao’ alisema Khan.
‘Lakini pia dhumuni la Zantel ni kuonyesha
kuwa kwa kufanya uwekezaji sahihi kila kitu kinawezekana, na hakika hilo
litajionyesha kwa vijana hawa ambao kwa mara ya kwanza toka mashindano ya BSS
yaanzishwe hawajawahi kusaidiwa kwa kiasi hiki’ alisisitiza Khan.
Kwa
upande wao washiriki watakaokuwa kwenye ziara hiyo wameishukuru kampuni ya
Zantel kwa kuwasaidia kurekodi nyimbo zao, kuzitangaza na sasa ziara hii.
‘Hakika Zantel wameonyesha utofauti na
makampuni mengine, kwani makampuni mengi hupotea baada ya kumalizika kwa shindano
au tukio husika, ila Zantel wamekuwa nasi baada ya kuisha mashindano
wakihakikisha tunarekodi nyimbo zetu na kuzitangaza, tunashukuru sana kwa hilo’
alisema Nsami Nkwabi, mmoja wa washiriki watakaokuwepo kwenye ziara hiyo.
Ziara
hii pia itawapa fursa kubwa Zantel na washiriki kutoa shukrani kwa mashabiki wa
mziki waliowaunga mkono wakati wa mashindano.
Kwa
upande wake mshindi wa Epiq BSS alisema mashabiki watarajie burudani kali
kutoka kwake,‘ nimejipanga sana kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania kuwa
hawakukokosea kunipigia kura niwe mshindi’ alisema Walter.
Wasanii
wengine watakaotoa burudani kwenye ziara hii ni Barnaba, Ben Paul, Linah na Ali
Nipishe.
No comments:
Post a Comment