Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 27, 2013

MILIONI 105 ZATUMIKA KUKARABATI JENGO LA HOSPITALI



Mkuu wa Wilaya ya Iringa akizundua Jengo la Utoaji wa Huduma ya Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (Picha zote na Denis Mlowe)
 Mkuu wa wilaya akiwa katika picha ya pamoja na madaktari na wahudumu wa hospitali ya rufaa |wa mkoa wa Iringa.
Na Denis Mlowe, Iringa
JUMLA ya shilingi Milioni 105 zatumika katika ukarabati wa Jengo la Huduma ya upasuaji wa Macho na kati ya hizo milioni 35 zitatumika kwa gharama ya kununulia vifaa vya tiba ya macho katika hospitali ya rufaa ya Iringa.
Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Leticia Warioba alisema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa uzinduzi wa Jengo la Huduma ya Upasuaji wa Macho na pamoja na Kituo cha Huduma ya Upimaji na kutengeneza miwani katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa  kwa udhamini wa mashirika ya Sightsaver na Brien Holder Vision kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioba alisema kwamba watumishi wa idara ya afya hususani upande wa macho kuzingatia kwamba wanatumia msaada huo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa manufaa ya wananchi na kuwataka wasimamizi wa huduma za afya hospitalini hapo kuhakikisha kuwa vifaa vyote vilivyotolewa na wadau kuingizwa katika leja ya Hosptali ya Mkoa.
“Vile vile vifaa hivi vitunzwe kwa kufanyiwa matengenezo na kinga kama inavyotakiwa ili viweze kutoa huduma kwa muda mrefu” alisema dk. Warioba na kuongeza kwamba “Ushirikiano ambao mashirika haya yameonyesha katika kuboresha huduma za afya ya macho ni mfano wa kuigwa na wadau wengine wa sekta za huduma za jamii”
Awali mratibu wa huduma ya macho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Dk. George Kabona alisema kwamba lengo la mradi huo ni kuhakikisha watu wote wenye upofu unaozuilika wanapata huduma na wale wenye upofu usiozuilika hasa watoto wanapata elimu bora kuhusu huduma za macho.
Alisema kwamba jumla ya watu 725 waliokumbwa na mtoto wa jicho walifanikiwa kufanyiwa operesheni toka mwaka 2009 hadi 2011 na opereshi  zote walifanyiwa watu 1265 kati ya wagonjwa 22,169 waliojitokeza ndani ya miaka mitatu ya 2009/2010/2011 aliongeza kusema kuwa mradi huo umewezesha kuwajengea uwezo watoa huduma wa macho mbalimbali ndani ya mkoa ikiwemo madaktari watatu wa upasuaji wa mtoto wa jicho ambao wawili wanatoa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
“Mradi umeweza kutoa elimu kwa wahudumu wengi wa afya ya msingi katika zahanati zetu ili waweze kutoa hudma nzuri za macho hasa maeneo ya vijijini ambako wataalam wa macho hawapatikaniki” alisema Dk. Kabona 
Mradi Jumuishi wa Huduma za macho mkoani Iringa ulianzishwa mwaka 1998 kwa kushirikiana kati ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa na Shirika lisilo la kiserikali la Sightsaver.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...