Wachezaji wa Libolo, wakishangilia baada ya kutupia bao lao katika dakika ya 24, kipindi cha kwanza.
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi
ya Klabu Bingwa Afrika, Simba, leo wamechapwa bao 1-0, dhidi ya Recreativo
Libolo ya Angola.
Mechi
hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Simba walibanwa
na wageni na kuruhusu bao pekee katika mchezo huo lililofungwa dakika ya 24 na
Joao Martins kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Carlos
Almeida.
Simba
ambao walianza mchezo kwa hofu huku wakiwaacha wageni kuutawala, ambapo dakika
ya saba wanaonana vizuri na Sidnei Mariano alipiga shuti kali lililogongwa
mwamba wa goli la Simba na kurudi uwanjani.
Dakika
ya 13, Simba walipata nafasi nzuri ya kufunga bao, lakini mpira wa krosi
uliopigwa na Nassor Chollo unakosa mmaliziaji na kuwapa nafasi
mabeki wa Libolo kuondosha hatari langoni kwao.
Libolo
wakicheza kwa kujiamini, akili na nguvu waliwadhibiti vizuri washambuliaji wa
Simba, Mrisho Ngassa na Haruna Moshi ‘Boban’, ambao walikuwa wakipelekwa
pembeni mara kwa mara.
Dakika
moja kabla ya mapumziko, kipa wa Simba, Juma Kaseja, alifanya kazi kubwa ya
kuokoa shuti kali la Carlos Almeida lililokuwa likielekea wavuni.Simba walikosa
bao la kusawazisha dakika ya 64, baada ya Boban, kushindwa kutumia vizuri pasi
iliyotoka kwa Haruna Chanongo, wakati tayari mpira ukiwa umewapita mabeki wa
Libolo.Beki aliyerejeshwa kundini Simba, Juma Nyosso, alijaribu kwenda mbele na
kufanya shambulizi la nguvu, lakini shuti lake la mguu wa kushoto lilipaa juu
ya lango la wapinzani wao.
No comments:
Post a Comment