Uongozi
wa mtandao wa sufiani mafoto blog umesikitishwa na vitendo
vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa blogs, kuwa wakiiba kazi za watu
katika blogs mbalimbali yaani ‘Kukopi na Kupaste’ kutoka katika blog
Fulani na kuweka katika Blogs zao bila kujali haki miliki ya kazi ya
mtu, wala kumpa haki yule aliyechukuliwa kazi yake kwa kuandika mahala
ilipochukuliwa kazi hiyo.
Kama
inavyojulikana utafutaji wa habari si lelemama na ikumbukwe ili kupata
habari iliyo bora na itakayowafurahisha wasomaji wako, kwenda na wakati
ni lazima uihangaikie na katika kuihangaikia kuna gharama kibao
zinazotumika, ikiwa ni pamoja na usafiri, pesa, na hata mafuta ya gari
kutoka mahala Fulani kwenda sehemu nyingine, gharama za simu na hata
kuwalipa wale unaowatuma ili kukufanyia kazi hiyo.
Kama
umeweza kufanya mambo yote hayo kwa gharama unazozijua wewe uliyeweka
stori, ama picha katika Blog yako, halafu watu wenye Blog Fulani wasio
na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua kazi yako kana kwamba ameokota tu
jalalani na anaweka kwake ili wasomaji wake wasome, bila kuwajulisha
kuwa kazi hiyo iliyomvutia imefanywa na mtandao Fulani kwa kweli
inaumiza, inaudhi na inarudisha nyuma malengo hasa ya kuwa na mitandao
hii, wote tutajaonekana wapuuzi.
Mtandao
huu umewavumilia watu hawa kiasi cha kutosha lakini sasa imezidi
kukithiri, kwani jamaa hawa wapo katika ukurasa wako kukusubiri kuona tu
ulichoweka kwa wakati huo, ili wao wakopi na kupaste kwao, halafu
tayari wamemaliza wala hawataki kujihangaisha kufanya kazi ili kuboresha
mitandao yao na kuwavutia wasomaji wao.
‘Unapoamua
kutangaza vita ujue tayari umeshajipanga kukabiliana na kila
litakalotokea mbele yako, na pia umejipanga katika kutoka upinzani wa
kweli ili watu waone na wakutambue, lakini sio kwa staili hii ya kuomba
mtangaziwe blog zenu kupitia kwa wale walioanza mapema halafu kumbe kazi
yenyewe ni kuchukua kazi za watu tu na si kufanya kazi’ yaani kukopi na
kupaste,
Kuna
msanii mmoja alichoshwa na wenzake wanaotamani kuingia kwenye gemu,
lakini wanashindwa kuumiza vichwa kubuni ili kuweza kupata radha
tofauti, na kuamua kuwafikishia ujumbe kwa kuwaimba kuwa ‘Si lazima wote
tuimbe kuna michezo mingi hata kucheza bao kama huwezi kuimba, ikiwa
kila wimbo unaotoka mpya umekopiwa, kama si mashahiri, basi ni Beat,
Na
hata katika mablogger si lazima wote tuwe na Mablogger, kama huwezi
kuumiza kichwa utoke vipi, basi kaa pembeni waachie wenye uwezo wa
kufanya kazi hiyo, kukopi na kupaste hadi mitandao yote inakuwa sawa
nini maana ya habari za haraka mtandaoni?,
Huoni kuwa mnawachosha wasomaji wenu, kwa kusoma habari na picha zinazofafa kwa wakati mmoja na katika mitandao yote?,
Tena
msomaji wako wakiwa ni waelewa hawawezi kusoma tena mtandao wako kwani
habari kama hiyo hiyo walikwishaiona katika mtandao Fulani muda mchache
uliopita na dakika chache baadaye wanaikuta vile vile walivyoisoma
kwingine ikiwa katika ukurasa wako, mara moja mara mbili msomaji huyo si
umempoteza?’’.
Mablogger
acheni uvivu na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu, na kama
ukifanya hivyo basi jitahidi kumpa credit yule uliyemchukulia kazi yake.
VITU
muhimu vy kuwa navyo ili kufanikisha kazi yako ya Blog, ni Laptop
‘Kompyuta mpakato’, ama Desk Top, Modem ‘Internet Wireless’, Kamera hata
ndogo tu ya mkononi, na pia ujue maana ya kuanzisha hiyo Blog yako na
malengo yako kwa jamii, kwani sidhani kama unaweza kuanzisha blog ili
uwe ukisoma mwenyewe na naniliu wako tu.
Na
kuwa na kamera si bora tu kuwa na kamera pia ujue kuitumia ipasavyo ili
kunasa picha nzuri uitakayo na itakayofikisha ujumbe kwa wasomaji wako
hata kwa kuiangalia tu, kwa kile ulichokusudia kuwaarifu wasomaji wako.
No comments:
Post a Comment