Philip Koyey akichapa makonde na bondia Kelly Brook wa Uingereza.
Nchi
ya Ghana iko katika hekaheka za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa
Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo
gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey.
Mabondia
wawili hao ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na
barani Afrika kwa ujumla, ambao watakutana wakati wanapogombea mkanda wa
IBF AMEPG uzito wa middle.
Muziki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye 'muziki wa masumbwi' ulingoni
wakati mabondia hao watakapokuwa wakionyeshana umwamba na
kuwadhihirishia mashabiki wa masumbwi katika bara la Afrika kuwa
wanasifa hizo kama wanavyotambulika.
Pambano hilo linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyakula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Makamu wa Rais wa IBF Africa idara ya fedha.
Kwa maana hiyo miamba hiyo inatarajia kukutana na kupanda jukwaani Machi 30,katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah.
Nchi
ya Ghana imetokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti
kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo
imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike
Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa wa ngumi kwa miaka kadhaa na
kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kufuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment