Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro,
alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwasalimiana na watoto wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro,
alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.
Mkazi
wa Kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi mjini, akionyesha kadi yake ya
matibabu ya Huduma ya Kadi ulkiopo chini ya Bima ya Afya, wakati wa
mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya
CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika kijiji hicho, leo Feb 16,
2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya kuzungumza wakati akihimiza
umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wa matibabu.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwa amegoma kushuka katika gari lake, kukataa kwenda kwenye mkutano wa
ndani wa Chama Kata ya Tandangongoro, uliokuwa umepangwa na viongozi wa
kata hiyo kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya msingi ya
kijiji cha Ng'apa, mkoani Lindi, leo Februari 16, 2013. Hatua hiyo
iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa dharura. Mama Salma
alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha siasa kufanyika katika
chumba cha darasa la shule ya serikali
Umati
wa wananchi wa Kijiji cha Ng'apa wakimsiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilipowahutubia mkutano
wa hadhara leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
No comments:
Post a Comment