Mkurugenzi
Mkuu wa Bendi ya Skylight Anneth Kushaba akizungumza na vyombo vya
habari jijini Dar es Salaam jana ambapo ametoa shukurani kwa mashabiki
na waandishi wa habari kwa kuiunga mkono bendi hiyo pamoja na kuwa bado
ni changa. Ameongeza kuwa bendi hiyo inapiga muziki aina ya ‘Afro Pop’
kutokana na falsafa yao ya muziki na mahitaji ya soko la muziki wa
‘Live’ hapa Tanzania. Kulia ni mwanamuziki Joniko Flower.
Kushaba amewataka mashabiki wa
muziki kuhudhuria kwa wingi katika show yao watakayopiga katika kiwanja
chao cha nyumbani cha Thai Village kuanzia saa tatu usiku.
Mwanamuziki
Joniko Flower wa Skylight Band akitoa kionjo kwa waandishi wa habari
waliohudhuria hafla fupi ya kutambulisha nyimbo mpya na kuwashukuru
mashabiki wao kwa kuwaunga mkono.
Aneth Kushaba AK 47 akiongoza kundi
la vijana wa Skylight Band kutoa burudani wakati wakitambulisha nyimbo
yao mpya ya "Nasaka Dhoughs" iliyomo kwenye albam yao yenye nyimbo nane
inayokaribia kutoka hivi karibuni.
Sam Mapenzi akijimwaga na sebene la Carolina.
Mwanamuziki Sony Masamba akikamua.
Salma Yusuf uzao wa BSS akionyesha kipaji chake kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa single mpya ya Skylight Band.
Na Mo Blog.
Kwa niaba ya bendi nzima ya Skylight
Mkurugenzi Mkuu Anneth Kushaba ameomba ushirikiano kutoka kwa
mashabiki, hamasa na kuungwa mkono katika kuendeleza burudani na kuleta
ladha mpya ndani ya fani ya Muziki.
Pia ameomba ushirikiano kutoka kwa
wadau mbalimbali ili kuendeleza juhudi za kuwahakikishia wapenzi
wanaohudhuria maonyesho yao Thai Village kila Ijumaa wanapata muziki
wenye kiwango bora kama unasikiliza CD.
Kushaba amesema wamefanikiwa kuboresha sauti kwa kuongeza aina ya vyombo vinavyotumika katika maonyesho ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment