Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 29, 2011

MABONDIA WA ZANZIBAR NA BARA KUONESHANA KAZI DDC KEKO KESHO

Alphonce Mchumiatumbo akipima uzito Dar es Salaam jana kwa ajili ya mpambano wake KESHO na Amour Zungu utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Keko leo kulia ni msimamizi wa mabondia hawo. Kanda Kabongo

LUDACRIS: NINAZO NYIMBO ZA KUTOSHA KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WANGU KATIKA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA JUMAMOSI

Mwanamuziki Ludacris kutoka nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika asubuhi hii kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dare es salaam, Ludacris alikuwa akizungumzia onyesho lake atakalolifanya kesho, katika tamasha la Mwendelezo wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwabja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, katika picha kulia ni Mkurugenzi wa radio Clouds Ruge Mutahaba. Ludacris amesema anazo albam saba hivyo katika albam hizo anatarajia kutoa burudani ya kutosha ili kukonga mioyo ya mashabiki wa wa muziki wake nchini Tanzania
Mwanamuziki Ludacris wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Ruge Mutahaba mkurugenzi Clouds kushoto ni Caroline Ndungu, aliyekuwa mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers na Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo.
Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungamza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati alipozunguzia tamasha la Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, katikati ni Mwanamuziki Ludacris na mwisho ni Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba.
http://fullshangwe.blogspot.com/

NANI KUIBUKA MSHINDI WA MISS ILALA LEO

REDDS MISS ILALA KUNYAKUA MILIONI 1.500.000 IJUMAA

Shindano la kumtafuta Mrembo wa Kanda ya Ilala linafikia kilele ijumaa wakati Walimbwende kumi na saba watakapo panda jukwaani kumenyana wakishindania Taji la Redds Miss Ilala ikiwa ni kwenye mchakato wa kuelekea kumpata Mrembo wa Tanzania.
Kila kitu kiko tayari kwa ajili ya Mashindano haya ambayo yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja. Warembo wamekamilika, maandalizi yote yako sawa sawa ikiwa ni kubadilisha kabisa maandhali ya viwanja vya Mnazi mmoja kutoka katika hali ya kuwa vya mikutano ya hadhara na kuwa katika hali ya viwanja vya starehe na burudani.
Michoro ya jinsi viwanja vitavyo onekana imetokana na Taman min Indonesia park iliyoko katika jiji la Jakarta na tunategemea kuwa kila atakayefika mahala pale atapata burdani tosha na kumfanya kuweka shindano la mrembo wa Ilala mwaka huu kuwa kumbukumbu kwake.
Bendi ya African Stars Twanga Pepeta itaanza kutumbuiza kuanzia saa moja kamili jioni na kutoa burdani kwa watu watakaokuwa wanaingia uwanjani hapo. Burdani pia itaporomoshwa na Mwanamuziki wa ngoma za asili Wanne Star na Warembo walioingia fainali katika Shindano la Vipaji.
Zawadi zitakazo tolewa kwa warembo ni kama ifuatavyo:
1. Redds Miss Ilala atapata Tshs 1,500,000/=
2. First Runner Up atapata Tshs 1,000,000/=
3. Second Runner Up atapata Tshs 850,000/=
Hawa watapata pia tiketi ya kuwakilisha Miss Ilala katika shindano la Vodacom Miss Tanzania.
4. Third Runner Up atapata Tshs, 500,000/=
5. Fourth Runner Up atapata Tshs. 500,000/=
6. Kifuta Jasho kila mmoja atapata Tshs 200,000/=

TENDE HIZOOOO MSIMU WAKE UHO EHEEE

Wafanyabiashara ya tende wakipima kwa kilo kwa ajili ya kuweka kwenye mifuko kuuza kushoto ni Sadam Mubaraq na Said Makingo kama walivyokutwa makutano ya mtaa wa Mafia na Swahili DAr es Salaam jana zao la tende upendwa kununuliwa sana katika kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani itakayoanza mwanzoni mwa mwezi ujao

Thursday, July 28, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGA MWILI WA MAREHEMU PROFESA MUSHI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick Sumaye, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa katika shughuli ya mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Profesa Mushi, na ndugu jamaa na marafiki, wakiwa katika shughuli za mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa Samuel Mushi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya marehemu.
Mtoto wa marehemu Profesa Samuel Mushi, Susan Mzee, akitoa shukrani kwa niaba ya familia ya marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick Sumaye, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA , WENJE ATOLEWA NJE, WABUNGE WASUTANA NJE YA BUNGE NUSURA KUCHOMANA VIDOLE VYA MACHO

Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge baada ya kutomtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba, alimtaka kukaa chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu Samaki wa sumu kutoka Japan. Picha Zote na Anna Nkinda-MAELEZO

Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge.

Baadhi ya mawaziri wakimpongea waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jummanne Maghembe mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya wizara yake jana jioni katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.

NJE YA UKUMBI WA BUNGE

Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na Mbunge wa viti Maalum (CHADEMA) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) baada ya Filikunjombe kumwambia, Ezekia Wenje, mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu Samaki wa sumu kutoka Japan.

Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti Maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) na Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini (NCCR – MAGEUZI) Moses Machari.

Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na baadhi ya wabunge wa upinzani Moses Machari (kulia), Philipa Mturano (katikati) na Ezekia Wenje (kushoto) baada ya Filikunjombe kumwambia Wenje kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.

Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto ) na Maryam Msabaha (katikati).

KATIBU WA NEC OGANAIZESHENI ASHA ABDALLAH JUMA AJULIA HALI MAJERUHI WA BASI LA HOOD NA KUKAGUA UHAI WA CHAMA MOROGORO

Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akimpa pole Beatrice Mjenga ambaye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi Mikumi, Morogoro
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma, akisalimia viongozi na wanachama wa CCM mkoa wa Morogoro kabla ya kuwahtubia katika ukumbi wa Vijana kwa ajili ya kuimarisha uhai wa Chama
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akihutubia viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro mjini Fikiri Juma.

CPWAA TO PERFORM ON BIG BROTHER AFRICA AMPLIFIED 2011 FINALE

Tanzanian Urban Music ( Bongoflava) Artist CP a.k.a CPwaa “ The King of BongoCrunk” has been invited by Big Brother Amplified/ MultiChoice Africa as one of the few selected artists in the continent to perform on the finale show 31st of July 2011. CPwaa will be the only artist from East Africa to represent live on the stage during the final BBA eviction show where one housemate will leave the house with a prize of 200,000 USD! Other invited Artist on the Big Brother Amplified Finale 2011 include WIZ KID and MO CHEDDA (Nigeria), FALLY IPUPA ( Congo) and South African’s PROFESSOR and SPEEDY.

Big Brother Amplified is Africa’s biggest Live show coming to its season end on 31st of July with over 50 Million viewers in 58 countries watching it live from their TV screens across the continent and the world. CPwaa is the second Tanzania artist to perform on BBA Amplified after “Shaa” who performed a couple of weeks ago. CPwaa also will be the second East African artist to perform on BBA Finale after WYRE ( Kenya) who performed on last year’s BBA finale. Other Artist who have been on the BBA stage 2011 include Cabo snoop ( Angola), Cindy (Zimbabwe),Vee and Scar (Botswana), EES (Namibia), AKA (South Africa), Ice Prince (Nigeria), Radio and Weasal ( Uganda), Nonini ( Kenya), Jaguar( Kenya) and Buster Rhymes( U.S.A). The finale will take place in Johannesburg, South Africa around 19.00 -21.00 EAT and broadcasted live through Channel 192/8 on DSTV Multichoice .

Cpwaa, the “ Action” song hit singer will perform his hit songs include ACTION featured Ms. Triniti, Dully Sykes and Mangwear. CPwaa’s team and management would like to thank all media houses and fans for supporting him and also thanks STREET SOUL CLOTHING RANGE for volunteering to sponsor CPwaa’s wardrobe for the whole trip.See CPwaa's latest video below and for more visit his official website:: http://www.cpwaa.co.tz/

Promosheni ya Bingwa, Dimba, Mtazania yachanja mbuga

NA MWANDISHI WETU
PROMOSHENI inayoendeshwa na Kampuni ya New Habari (2006) Limited, watengenezaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania, The African na Rai, inayojulikana kwa jina la Mchongo, imezidi kushika kasi ambapo wasomaji wa magazeti ya kampuni hiyo, wanazidi kujitokeza kuchangamkia promosheni hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko na Usambazaji wa New Habari (2006) Ltd, Grace Kassella, kila siku wamekuwa wakipokea kuponi lukuki za ushiriki wa promosheni hiyo inayomwezesha msomaji wa Bingwa na Dimba kujishindia gari aina ya Toyota Vitz na Suzuki Escudo kwa wasomaji wa gazeti la Mtanzania.
Alisema kuwa wamefurahishwa kuona kuwa hata wasomaji wao wa mikoani, wamejitokeza kwa wingi kujaza kuponi za promosheni hiyo na kuzituma kwao.
“Hili ni jambo la kufurahisha, kuona hata wasomaji wa mikoani wamepata mwamkoa wa kushiriki pro mosheni hii ambayo mbali ya kujishindia gari katika droo kubwa itakayofanyika baada ya miezi mitatu, pia kutakuwa na zawadi za kila mwezi za luninga, fulana, miamvuli, mipira, jezi, ambati na saruji,” alisema.
Aliwataka wasomaji wa Bingwa, Dimba na Mtanzania kuchangamkia kwa wingi promosheni hiyo kwa kujaza kuponi iliyopo ukurasa wa pili wa magazeti hayo na kuzituma makao makuu ya kampuni hiyo, yaliyopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Grace amesema kuwa wanatarajia kuitangaza promosheni hiyo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wakianzia na Mwanza, Arusha, Morogoro, Tanga na Mbeya.
“Kwa sasa hapa Dar es Salaam tunafanya matangazo ya mitaani kuitangaza promosheni hii, lakini pia kuwatangazia wasomaji wetu ubora wa magazeti na bidhaa zote zinazozalishwa na New Habari…sasa tumeona ni vyema tukafanya hivyo na mikoani ili tuweze kuwapa wasomaji wetu fursa ya kuifahamu zaidi promosheni hiyo pamoja na ubora wa bidhaa zetu,” alisema.
New Habari (2006) Limited, ni miongoni mwa kampuni kongwe za habari hapa nchini, huku gazeti la Bingwa likiwa ndilo gazeti pekee la michezo na burudani linalotoka kila siku, wakati Dimba likiwa ni gazeti bora kabisa la michezo na burudani linalotoka mara mbili kwa

TIGO YASAIDIA SHULE DAR ES SALAAM

Msimamizi wa biashara na Masoko wa Kampuni ya TigoBw.Gaudens Mushi akizungumza na mtoto wa darasa la pili shule ya msingi Msisiri Hifta Jafari wakati kampuni hiyoilipokwenda kugawa madawati ya mapajani
Wanafunzi wa shule ya msingi msisiri wakiwa na madawati ya mapajani baada ya kukabidhiwa
Gaudens Mushi akimkabidhi madawati ya mapajanimwalimu mkuuwa wa shule ya msingi msisiri Bi.Prisca Myalla wanaoshughudia ni mwalimu Anna Lyatu na Mwenyekiti wa Shule hiyo Bw.Joseph Shay

Wednesday, July 27, 2011

JOACHIMU CHISANO ATEMBELEA WAKULIMA WA ZAO LA MLONGE BAGAMOYO

Joachim Chissano akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Bi,Eileen Kasubi
Bi,Eileen Kasubi katikati akiwa katika shamba la zao la mlonge na mgeni wake Joachim Chissano

Joachim Chissano kushoto akitembezwa katika shamba la zao la mlonge na mwenyeji wake Eileen Kasubi

Rais Mstaafu wa Msumbiji, Bw. Joachim Chisano kushot
o akitoa neno la shuklani baada ya kutembelea katika shamba la zao la mlonge

joachim Chissaibishwano akikao

WAZIRI WA MAWASILIANO RWANDA AZURU ZANTEL

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya yeye na Waziri wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano wa Rwanda, Dk. Ignace Gatare (katikati) kufanya ziara ya kikazi kukagua mitambo ya mkonga wa mawasiliano wa EASSy uliopo Makao Makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Norman Moyo. Afisa Mkuu wa Kiufundi wa Zantel, Moncef Mettiji (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano wa Rwanda, Dk. Ignace Gatare wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua mitambo ya mkonga wa mawasiliano wa EASSy uliopo Makao Makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Norman Moyo (aliyenyoosha mkono kulia) akitoa mada kuhusu mkongo wa mawasiliano wa EASSy iliopo kwenye makao makuu kampuni hiyo. www.johnbadi.blogspot.com

SUPER NYAMWELA KUTOKA NA RAP MPYA YA 'NASAKA MAHELA' NDANI YA EXTRA BONGO

Mnenguaji mahiri wa bendi ya Extra Bongo ‘Super Nyamwela’ yupo mbioni kuipua rap yake mpya inayokwenda kwa jina la Nasaka Mahela, atakayoitumia katika wimbo mpya uliotungwa na Roggat Hegga Katapila uitwao Ufisadi wa Mapenzi.

Akizungumza na Mtandao huu wa Sufianimafoto, Nyamwela alisema kuwa, wimbo huo umerekodiwa katika Studia ya Sofia Records utakaotoka sambamba na video yake ambayo pia itarekodiwa katika studio hiyo.

Aidha Nyamwela alisema kuwa pia katika albam mpya ijayo ya bendi hiyo atakuwa na kibao chake alichotunga mara tu baada ya kutua katika bendi hiyo akitokea African Stars Twanga Pepeta, ambao bado unaendelea kufanyiwa mazoezi na wanamuziki wa bendi hiyo.

Bendi hiyo ya Extra Bongo iliyo chini ya Mkurugenzi wake Ally Choki, ipo katika maandalizi ya albam yao mpya inayotarajia kukamilika hivi karibuni.
Mnenguaji Super Nyamwela ambaye pia ni kiongozi wa Safu ya wanenguaji wa bendii ya Extra Bongo (kulia) akishambulia jukwaa pamoja na wanenguaji wenzake katika moja ya onyesho lao lililofanyika hivi karibuni
http://sufianimafoto.blogspot.com/

JAKAYA AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUMBUKUMBU YA KUWAENZI MASHUJAA WETU

Askari walikuwa wakikusanyika kwa kusikia mlio wa King'ora hiki cha
kuzungusha kwa mkono.
BEATRICE MLYANSI NA JOSEPH ISHENGOMA, MAELEZO-MTWARA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana aliwaongoza mamia ya wananchi katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa iliyofanyika kitaifa katika makaburi ya mashujaa Naliendele mkoani Mtwara.
Baada ya kuwasili katika makaburi hayo ya mashujaa, Mhe.rais aliweka silaha za asili ambazo ni mkuki na ngao katika mnara wa kumbukumbu za mashujaa.
Mzee Ernest Waya, mkazi wa mkoani Mbeya akiweka upinde na mshale katika Mnara wa mashujaa uliopo mkoani Mbeya, kuwakumbuka wapiganaji wenzake aliokuanao katika Vita Kuu ya pili ya Dunia. Ernest , ameitaka Serikali kuwakumbuka wazee hao na si kukumbukwa siku ya maadhimisho hayo pekee ambayo hufanyika mwaka hadi mwaka.
Kifaa cha Mawasiliano kilichokuwa kikitumiwa na askari wetu.
Aidha mkuu wa majeshi ya Usalama na Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange aliweka sime, Kiongozi wa Mabalozi nchini Balozi Juma Alfani Mpango aliweka shada la maua,wakati Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Selemani Mtalika Shiringi aliweka upinde na mishale na Kiongozi wa Tanzania Legion Ezekiel Chacha aliweka shoka.
Kisha viongozi wa dini wakiongozwa na Sheikh Jamaldin Salim Chamwi alisoma dua kwa niaba ya Waislamu ,Mchungaji Lucas Mbedule alisoma sala kwa niaba ya Jumuiya ya Wakristu Tanzania na Mhasham Askofu Gabriel Mmola alisoma sala kwa niaba ya Wakatoliki.
Baada ya sala hizo Mhe.Rais alitembelea makaburi na kisha kuwasalimia wananchi na kuwashukuru wananchi kwa kufika katika sherehe hizo muhimu kitaifa na kusema “Lengo la Sherehe hizi ni kusherehekea maisha ya mashujaa sio kufa kwao.”
“ Lengo la sherehe hizi ni kusherehekea maisha ya mashujaa sio kufa kwao,.Mashujaa hawa walilipa gharama kubwa kwa kutoa uhai wao kwa nchi yao”alisema Rais Kikwete.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Eng.Felipe Jacinto Nyusi alitoa shukrani kwa Tanzania kwa niaba ya nchi yake jinsi ilivyosaidia kuleta amani na utulivu nchini mwake.
“Nawashukuru sana watanzania maana uhuru wetu umetoka hapa,sasa tumetulia nyumbani kwa sababu ya damu iliyotulia hapa Naliendele.”alisema Waziri Nyusi.
Moja ya silaha iliyotumiwa na askari wetu katika kutafuta Ukombozi
wa watu wa Msumbiji
Viongozi wengine wa kitaifa waliohudhuria maadhimisho hayo ni makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal ,Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali.
Sherehe hizi ni za pili kufanyika nje ya jijini la Dar es salaam ambapo mwaka 2009 zilifanyika katika makaburi ya Kaboya mkoani Kagera.

Hili ni moja kati ya Majeneza yaliyotumika kubebeba masalia ya Miili ya askari wetu na kuwasafirisha kutoka Msumbiji kuja Tanzania
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...