NA MWANDISHI WETU
PROMOSHENI inayoendeshwa na Kampuni ya New Habari (2006) Limited, watengenezaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania, The African na Rai, inayojulikana kwa jina la Mchongo, imezidi kushika kasi ambapo wasomaji wa magazeti ya kampuni hiyo, wanazidi kujitokeza kuchangamkia promosheni hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko na Usambazaji wa New Habari (2006) Ltd, Grace Kassella, kila siku wamekuwa wakipokea kuponi lukuki za ushiriki wa promosheni hiyo inayomwezesha msomaji wa Bingwa na Dimba kujishindia gari aina ya Toyota Vitz na Suzuki Escudo kwa wasomaji wa gazeti la Mtanzania.
Alisema kuwa wamefurahishwa kuona kuwa hata wasomaji wao wa mikoani, wamejitokeza kwa wingi kujaza kuponi za promosheni hiyo na kuzituma kwao.
“Hili ni jambo la kufurahisha, kuona hata wasomaji wa mikoani wamepata mwamkoa wa kushiriki pro mosheni hii ambayo mbali ya kujishindia gari katika droo kubwa itakayofanyika baada ya miezi mitatu, pia kutakuwa na zawadi za kila mwezi za luninga, fulana, miamvuli, mipira, jezi, ambati na saruji,” alisema.
Aliwataka wasomaji wa Bingwa, Dimba na Mtanzania kuchangamkia kwa wingi promosheni hiyo kwa kujaza kuponi iliyopo ukurasa wa pili wa magazeti hayo na kuzituma makao makuu ya kampuni hiyo, yaliyopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Grace amesema kuwa wanatarajia kuitangaza promosheni hiyo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wakianzia na Mwanza, Arusha, Morogoro, Tanga na Mbeya.
“Kwa sasa hapa Dar es Salaam tunafanya matangazo ya mitaani kuitangaza promosheni hii, lakini pia kuwatangazia wasomaji wetu ubora wa magazeti na bidhaa zote zinazozalishwa na New Habari…sasa tumeona ni vyema tukafanya hivyo na mikoani ili tuweze kuwapa wasomaji wetu fursa ya kuifahamu zaidi promosheni hiyo pamoja na ubora wa bidhaa zetu,” alisema.
New Habari (2006) Limited, ni miongoni mwa kampuni kongwe za habari hapa nchini, huku gazeti la Bingwa likiwa ndilo gazeti pekee la michezo na burudani linalotoka kila siku, wakati Dimba likiwa ni gazeti bora kabisa la michezo na burudani linalotoka mara mbili kwa
No comments:
Post a Comment