KUMB.Na:GS/PPAT/01/2011 7 Julai ,2011
MHARIRI WA HABARI
………………………………
Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na watanzania wote kulaani kitendo cha Kinyama alichofanyiwa Mpigapicha wa Gazeti la Majira na Mwandishi wa Sani, kwa kuvamiwa na wananchi, kupigwa na kuporwa mali zao wakati wakiwa kazini kuripoti tukio la vurugu za kundi la vijana waliokuwa wakishambulia polisi kwa mawe baada ya Polisi kuchukua Mwili wa Marehemu Bakari Hamisi ambaye ndugu zake waligoma kuu zika Julai 6, 2011 huko Manzese Dar es Salaam.
Kitendo walicho fanyiwa Wanahabari hao ni cha Kinyama na katu hakiwezi kuvu milika.
Hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ipasavyo na kuhakikisha wote waliofanya vurugu hizo wanapatikana na kufunguliwa mashitaka kwa vitendo hivyo vya vurugu na kujeruhi watu na kuharibu mali.
Kumekuwapo na vitendo vingi vya kinyama wanavyofanyiwa Waandishi wa Habarui hasa Wapigapicha kwa kupigwa na wananchi ama Polisi ambao kimsingi wanajua kazi na wajibu wa Wanahabari katika jamii.
Pia hivi karibuni, katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Mpigapicha wa Mwananchi Communication Fidelis Felix akiwa kazini alishambuliwa na kuharibiwa Camera yake na Askari.
PPAT inapenda kuliomba Jeshi la Polisi kutoa elimu kwa Askari wake kuwa Mwandishi wa Habari si mtu wa kubugudhiwa na kupigwa wakati wanafanya kazi zao kwani kufanya hivyo ni kuinyima haki jamii kupata habari mbalimbali zinazo tokea katika jamii.
PPAT inawapa pole Heri Shabani na Christopher Lissa kwa mswaibu yaliyowafika na Mungu awape nguvu na kurejea tena katika kazi.
MHARIRI WA HABARI
………………………………
YAH: TAMKO LA PPAT KULAANI KUSHAMBULIWA KWA MPIGAPICHA HERI SHABANI WA GAZETI LA MAJIRA NA MWANDISHI CHRISTOPHER LISA WA SANI.
Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na watanzania wote kulaani kitendo cha Kinyama alichofanyiwa Mpigapicha wa Gazeti la Majira na Mwandishi wa Sani, kwa kuvamiwa na wananchi, kupigwa na kuporwa mali zao wakati wakiwa kazini kuripoti tukio la vurugu za kundi la vijana waliokuwa wakishambulia polisi kwa mawe baada ya Polisi kuchukua Mwili wa Marehemu Bakari Hamisi ambaye ndugu zake waligoma kuu zika Julai 6, 2011 huko Manzese Dar es Salaam.
Kitendo walicho fanyiwa Wanahabari hao ni cha Kinyama na katu hakiwezi kuvu milika.
Hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ipasavyo na kuhakikisha wote waliofanya vurugu hizo wanapatikana na kufunguliwa mashitaka kwa vitendo hivyo vya vurugu na kujeruhi watu na kuharibu mali.
Kumekuwapo na vitendo vingi vya kinyama wanavyofanyiwa Waandishi wa Habarui hasa Wapigapicha kwa kupigwa na wananchi ama Polisi ambao kimsingi wanajua kazi na wajibu wa Wanahabari katika jamii.
Pia hivi karibuni, katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Mpigapicha wa Mwananchi Communication Fidelis Felix akiwa kazini alishambuliwa na kuharibiwa Camera yake na Askari.
PPAT inapenda kuliomba Jeshi la Polisi kutoa elimu kwa Askari wake kuwa Mwandishi wa Habari si mtu wa kubugudhiwa na kupigwa wakati wanafanya kazi zao kwani kufanya hivyo ni kuinyima haki jamii kupata habari mbalimbali zinazo tokea katika jamii.
PPAT inawapa pole Heri Shabani na Christopher Lissa kwa mswaibu yaliyowafika na Mungu awape nguvu na kurejea tena katika kazi.
Mwasiliano zaidi
0717002303/0755 373999
0717002303/0755 373999
Mroki Mroki
Katibu Mtendaji PPAT.
No comments:
Post a Comment