Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 14, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 3 WA BARAZA LA WAKUU WA VYUO VIKUU HURIA AFRIKA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria cha Zanzibar Tanzania, Grace Kissassi, wakati alipokutana naye baada ya kufungua rasmi mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika, kuhusu elimu ya mafunzo ya masafa uliofunguliwa rasmi leo Julai 13, 2011 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa siku 3, kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa unaowashirikisha wakuu wa Vyuo Vikuu Huria kutoka nchi za Afrika, uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika baada ya kuzindua mkutano huo kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa, leo Julai 13 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini wakifuatilia hotuba ya Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa mkuu wa tatu wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu kuhusu Elimu ya mafunzo ya Masafa uliofunguliwa lei Julai 13 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...