Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari, mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuwatembeza wahariri wa vyombo vya habari, ili kujionea mitambo mipya ya kiwanda cha kampuni ya bia ya Serengeti SBL, kilichojengwa maeneo ya Bomambuzi mjini Moshi. Wahariri hao wametembelea kiwanda hicho ikiwa ni kukalimisha ratiba ya mambo mbalimbali ambayo walijipangia, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa jukwaa la wahariri uliomalizika leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha. Katika jukumu lingine walilokuwa nalo ilikuwa ni kucheza mchezo mmoja wa mpira wa miguu kati yao na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti, ambapo mchezo huo umechezwa katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi CCP na timu hizo kutoka suluhu ya magoli 0-0, baadae usiku huu wataingia katika tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi.
Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication na mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Theophil Makunga kulia na Mkurugezi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda wakitoka nje. mara baada ya kuzitumikia timu zao katika mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu, uliofanyika uwanja wa Ushirika Moshi na timu hizo kutoka sare ya 0-0.
Mmoja wa wachezaji wa timu ya Serengeti akiwatoka mabeki wa timu ya Jukwaa la Wahariri katika mchezo wao, uliofanyika katika uwanja wa Ushirika Moshi leo jioni.
Mchezaji mwa timu ya Serengeti Breweriers Teddy Mapunda akiukokota mpira kuelekea goli la wapinzani wao timu ya Jukwaa la Wahariri.
Kikosi cha JUkwaa la wahariri kikijifua kushoto anayekiongoza ni Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Theophil Makunga.
Kikosi cha Serengeti Breweriers kikiwa katika picha ya pamoja kikongozwa na mshabuliaji wake Teddy Mapunda wa pili kutoka kulia mstari wa mbele.
Mgeni rasmi katika mpambano huo ambaye pia ni Mhariri mkuu wa Gazeti la Habari Leo Joseph Kulangwa, akisalimiana na mshabuliaji wa timu ya Serengeti Breweriers ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda kabla mchezo huo haujaanza, kulia ni kocha wa timu ya Jukwaa la Wahariri na mhariri wa Spoti Starehe Masoud Sanane.
No comments:
Post a Comment