Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 4, 2012

MAMA PINDA AENDESHA KAMPENI YA SAIDIA TAIFA QUEENS



Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group ,Bw.Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake, Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Tunu Pinda mara alipowasili mapema leo asubuhi kwenye ofisi hizo.
Mke wa waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (pili kulia) akiwa amepozi katika picha ya pamoja na Watangazaji wa kipindi cha Power breakfast kutoka Clouds FM mapema leo asubuhi, Mama Pinda alifika kwenye ofisi za redio hizo kwa ajili ya kuwahamasisha jamii mbalimbali kuisaidia timu ya Taifa Queens kwenye michuano yake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni hapa jijini dar. Kutoka kulia ni Gerald Hando, Barbla Hassan pamoja na Paul James.

Mama Tunu Pinda akiwa ni mmoja wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali wameamua kushiriki kuihamasisha jamii na wadau mbalimbali kuisaidia timu ya mpira ya wanawake ya Netboli (Taifa Queens ) kuhakikisha inafanikisha malengo yake na pia kuhakikisha maandalizi yote yanakwenda sawa. Pichani ni Mama Tunu Pinda akizungumza leo kwenye kipindi cha Power breakfast kupitia redio ya Clouds FM jijini Dar kuhusiana na mchakato mzima wa kuisadia Taifa Queens,kulia ni Paul James a.k.a PJ.

Taifa Queens kwa sasa iko kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashidano ya Netiboli ya Kombe la Afrika, ambapo Tanzania kupitia CHANETA imepewa heshima ya kuandaa Mashindano ya Netiboli ya Kombe la Afrika ambayo yanatarajiwa kuanza Mei 8-12, mwaka huu. Mama Tunu Pinda aliweka bayana kuwa gharama za kuendesha mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 127.


Hivyo Mama Pinda amewaomba wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kufanya vyema kwenye michuano yake,aidha amewataka Wadau watakaokuwa na nia kuichangia timu hiyo basi watume michango yao kupitia namba ya simu 0779 000 808 (huduma ya Easy pesa),ambapo mtu ama kampuni anaweza kutuma kwenye namba hiyo kwa mitandano yote.
Picha: Michuzijr Blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...