Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 4, 2012

MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA APOKEA MICHANGO YA TAIFA QUEENS



MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda jana amepokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwitikio wa ombi lake kwa Watanzania kuwaomba waichangie timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens) ili iweze kushiriki Mashindano ya Kombe la Afrika mwezi ujao.
Mama Tunu Pinda amepokea simu ya mtandao wa Zantel namba 0779-000-808 ambayo imeunganishwa na huduma ya EZY-PESA. Simu hiyo ambayo imekabidhiwa kwa uongozi wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) inawawezesha Watanzania kutuma pesa kwenye namba hii kutoka mitandao yote ya simu.


Meneja Mawasiliano wa Zantel, Bi. Awaichi Mawalla alitumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kutuma michango yao kupitia namba hiyo ili heshima ya Tanzania ambayo imepewa jukumu la kuandaa mashindano ya Kombe ya Afrika isitetereke.


Tanzania kupitia CHANETA imepewa heshima ya kuandaa Mashindano ya Netiboli ya Kombe la Afrika ambayo yanatarajiwa kuanza Mei 8-12, mwaka huu. Gharama za kuendesha mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 120.

(Mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMANNE, APRILI 3, 2012.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...