Wachezaji wa timu nya taifa ya Nigeria 'Super Eagles' wakishangilia
kutinga nusu fainali ya AFCON 2013 kwa kuichapa Ivory Coast mabao 2-1.
RUSTENBURG, Afrika
Kusini
TIMU ya soka ya taifa ya Ivory ‘The Elephant’, leo
imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Nigeria ‘Super Eagle’ na kuaga rasmi
fainali za Mataifa Afrika ‘AFCON 2013’ zinazoendelea kushika hapa.
Ivory Coast moja ya mataifa yaliyokuwa yakipewa nafasi kubwa
ya kutwaa ubingwa wa michuano ya mwaka huu, ilishutushwa na bao la mshambuliaji
wa Spartak Moscow, Emmanuel Emenikre katika dakika ya 42, lililowapeleka
mapumziko wakiwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, ambapo Tembo wa Ivory
Coast walifanikiwa kusawazisha kupitia kiungo nyota wa Newcastle United, Cheik
Tiote dakika ya 49 na kuamsha shangwe za mashabiki wa timu hiyo waliojazana
kwenye dimba la Royal Bafokeng.
Alikuwa ni Sunday Mba wa Enugu Rangers ya Nigeria, aliyeipa
bao la ushindi kunako dakika ya 77 ya mchezo huo na kuivusha hadi nusu fainali
na kuirejesha nyumbani Ivory Coast ambayo mwaka jana ilitinga fainali
ilikolazwa kwa changamoto za mikwaju ya penati na Zambia.
Kwa ushindi huo, Nigeria sasa itacheza nusu fainali kwenye
Uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban hapo Februari 6, kuwavaa Mali, ambao juzi
usiku waliwang’oa wenyeji Afrika Kusini kwa penati 3-1 baada ya sare ya 1-1
katika dakika 120 za mchezo huo.
Akizungumzia mechi
hiyo, kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi alisema:
"Mimi kwa dhati ya moyo wangu ningependa kuwashukuru
wachezaji wangu kwa kila kitu walichokifanya leo katika mechi hii. Nina
matumaini kwamba kwa mtindo huu tutasonga hatua kwa hatua hadi fainali.
"Ivory Coast ni timu bora na kinara wa bara zima,
iliyosheheni nyota kila idara na kimsingi tulijaribu kuwakimbiza na kuwakamata
nyota wao kama Drogba na Yaya Toure.
"Nina furaha na aina ya ukomavu unaooneshwa na vijana
wangu katika kila mchezo. Kumekuwa na nidhamu ya hali juu kikosini nah ii inanipa
matuamini ya kusonga mbele zaidi na zaidi.
"Vijana walionesha umakini na utulivu, hata Ivory coast
waliposawazisha, tulihakikisha tunajilinda vema huku tukisaka bao la ushindi na
kweli tukafunga tena na kukamilisha Jumapili nzuri nay a aina yake."
Kwa upande wake kocha wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi alisema:
"Najivunia aina ya wachezaji nilionao na kazi
waliyofanya.
"Bila shaka lengo letu kama timu ililikuwa kutwaa taji
na kama ujuavyo hii inaweza kuwa fursa ya mwisho kwa nyota wengi kikosini na
nadhani hii itatuumiza mn katika vyumba vya kuvalia, lakini ndio soka. Hakuna geni
lililotukuta.
"Ni huzuni kubwa kwangu mimi kama ilivyo kwa wachezaji
ambao walifanya lkazi kubwa wakilenga kutwaa ubingwa wa Mataifa Afrika – llakini
jitihada hazikutosha kutuwezesha kufanmikisha hilo."
…….SuperSport.com……
No comments:
Post a Comment