Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 18, 2011

FILAMU YA SHOGA YAPIGWA STOP MTAANI


MWANDAAJI wa Filamu, Hisani Muya, maarufu kama, 'Tino', amesema kuwa amesikitishwa na Wizara kuizuia filamu yake ya Shoga, aliyoikamilisha na kuizindua siku za hivi karibuni.
Akizungumza na Sufianimafoto, kwa njia ya simu, alisema kuwa amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa kutokana na kuwa tayari amekwishatumia gharama kibao katika kuiandaa ikiwa ni pamoja na uzinduzi uliofanyika Februari 4 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema kuwa alikuwa tayari akifanya maandalizi ya kwenda kuizindua Jijini Mwanza, lakini kutokana na agizo hilo la wizara imembidi asubiri majibu ya Wizara hiyo kuwa aendelee na utaratibu ama la na kuwa anahitaji kuifanyia marekebisho katika sehemu gani.
"Lakini iwapo watasema kuwa haifai basi nitawasikiliza ila tayari nitakuwa nimeshapata hasara ya kuiandaa hadi ilipofika.

AGIZO LA WIZARA
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeiagiza Kampuni ya kutengeneza filamu ya 'Al-Riyamy Production Company' kuwasilisha Filamu ya 'Shoga' kwa Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu kwa ajili ya ukaguzi.

Aidha Kampuni hiyo pia imeagizwa kutoisambaza Filamu ya 'Shoga' na kusitisha hatua nyingine yoyote kuhusiana na filamu hiyo hadi hapo Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu itakapojiridhisha kuwa filamu hiyo inakidhi kuonyeshwa hadharani kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Filamu na Michezo ya Jukwaani Namba 4 ya mwaka 1976.

Kampuni hiyo inatakiwa kuwasilisha kanda hiyo kabla ya tarehe 17 februari, 2011, Kwa mujibu wa Sheria hiyo hairuhusiwi kutengeneza filamu bila kupata kibali cha kutengeneza filamu.

Aidha kifungu cha 4 (1) kinaelekezwa bayana kuwa kila anayetengeneza filamu anatakiwa kuwasilisha maombi kwa maandishi kwa Waziri chini ya Sheria hii yakiambatana na mswaada na maelezo ya filamu inayotarajiwa kutengenezwa.
Pamoja na mambo mengine katika kifungu cha 14 (2) Sheria inaipa Bodi ya Filamu mamlaka ya kukagua filamu, picha ya matangazo au maelezo yake kwa makusudi ya kuamua kuonyesha na ikiwarushusu itatolewa maonyesho yawe kwa
namna gani.
Katika Sheria hiyo kifungu cha 15 (1) kinapiga marufuku kwa mtu yoyote kuongoza, kusaidia , kuruhusu au kushiriki katika maonyesho ya filamu bila kuwa na kibali cha Bodi.Sheria hii ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa waraka Namba 22 wa mwaka 1974.

Imetolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na MawasilianoWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tarehe 14 februari,2011.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...