Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 9, 2011

MASHINDANO YA NYAMA CHOMA YAZINDURIWA

Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Buttallah (kati) akifafanua jambi wa wakti wa uzinduzi wa mashindano ya kuchoma nyama yajulikanayo kama "Safari Lager Nyama Choma"katika pub iliyopo ndani ya kampuni ya bia Tanzania,jijini Dar.kulia na kushoto ni majaji wa mashindano hayo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi yale mashindano ya aina yake na ya kuvutia ya kuchoma nyama yajulikanayo kama “Safari Lager Nyama Choma”

Mashindano haya hushirikisha majiko ya baa mbalimbali katika umahiri wa kuchoma nyama na hatimaye zawadi hutolewa kwa washindi.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu, meneja wa Bia ya Safari Lager Bw. Fimbo Butallah alisema; madhumuni makubwa kwa bia ya Safari lager kuendesha mashindano haya ambayo yamekuwa kivutio kwa walaji wa nyama na watumiaji wa bia ni kuhakikisha tunaleta changamoto kwa majiko yanayochoma nyama, ili kuhakikisha walaji wanapata kile kilicho bora kabisa. Watumiaji wa bia ya Safari Lager, hupendelea sana kuitumia huku wakisindikiza na nyama choma iliyoandaliwa vizuri, hivyo kupitia mashindano haya, bia ya Safari Lager inaendeleza utamaduni wa kunywa bia na kula nyama. Kufuatia ubora wa hali ya juu wa bia ya Safari lager, tunafurahi sana pale ambapo mywaji atapata pia nyama iliyo bora ili mtumiaji aweze kuridhika zaidi.

Mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika mikoa mine ambayo ni; Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya. Kuna ongezeko la mkoa wa Mbeya ambao mwaka juzi haukushiriki. Ni matarajio ya bia ya Safari Lager kuyapeleka mashindano haya katika mikoa yote siku za usoni.

Akitaja zawadi za washindi, Butallah alisema; baa itakayoshika nafasi ya kwanza itajinyakulia shilingi Milioni Moja, mshindi wa pili, Laki Nane, Mshindi wa Tatu laki Sita, Nafasi ya Nne; Laki Nne na nafasi ya Tano shilingi Laki Mbili. Zawadi hizi zimegawanywa kwa kila mkoa.

Utaratibu wa kupata baa zitakazoshiriki mashindano haya utaendeshwa kwa njia ya simu, ambapo wananchi watatakiwa kutuma ujumbe mfupi usemao “Safari kisha Mkoa uliopo ikifuatiwa na jina la Baa” kisha tuma kwenda namba 15540. Utapokea ujumbe kukuhakikishia kuwa kura yako imepokelewa. Jopo la majaji litapitia kura zote na Baa Tano zitakazokuwa zimepata alama za juu zaidi ndizo zitakazopambana katika eneo la wazi ambapo mandhari ya kula nyama na kunywa bia itakuwa imeandaliwa.

Vigezo vitakavyoangaliwa na majaji katika mashindano haya ni pamoja na Usafi wa eneo, vifaa na muhusika, uchaguzi wa nyama, maandalizi ya nyama, jinsi ya uchomaji, muda unaotumika, jinsi nyama inavyofikishwa kwa mlaji na Ladha. Baa zitakazofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro zitapewa semina elekezi juu ya vigezo hivi kabla ya mpambano.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...