Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 4, 2011

WATU MIA MOJA KUPIMWA MACHO NA KUFANYIWA UPASUAJI BULE


JUMUIYA ya Mabohora nchini itafanya upasuaji wa macho bure ikiwa ni maadhimisho ya kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa shekhe wao Dkt. Syedna Mohammed Burhanuddin.

Mjumbe wa Kamati ya maadhimisho hayo, Bw. Saifuddin Jamal alisema jana kuwa watu wote wenye matatizo ya macho wanatakiwa kujiorodhesha katika hospitali za Amana, Temeke, Mwananyamala na Amtulabai ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Bw. Jamal alisema wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ni 100 kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam watakaowahi kujiandikisha katika hospitali hizo zilizotajwa baada ya kuidhishwa na madaktari wa hospitali hizo.

"Waliogundulika kuwa wana matatizo ya macho ya mtoto wa jicho na presha ya macho watafanyiwa upasuaji Februari 7 hadi 10 kwenye hospitali ya Burhani na daktari Dkt. Mustafa Parekt kutoka India anayetarajia kuwasili kesho kutwa (Jumapili)". alisema.

Alisema wenye matatizo hayo yanaweza pia kujiandikisha katika hospitali ya Burhani ambako upasuaji huo utafanyika kwa wastani wa wagonjwa 25 kwa siku.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...