Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 6, 2011

WATANZANIA TUMSAIDIE MZEE KIPARA

Na Mwandishi Wetu UNAMFAHAMU muigizaji mkongwe anayekwenda kwa jina la ‘Mzee Kipara?” Kama jibu ni ndiyo basi soma habari hii. Mzee Kipara ambaye jina lake halisi ni Saidi Fundi (pichani) hivi sasa anasumbuliwa na miguu kukosa nguvu, tatizo ambalo endapo atapelekwa hospitali pengine linaweza kupata nafuu kama si kupona kabisa. Kampuni ya Global Publishers inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi imempa simu ya mkononi msanii huyo mkongwe, ambayo itamsaidia katika mawasiliano na wasamaria wema ambao tunawaomba mumchangie kwa njia yoyote hasa ya M-Pesa. Simu hiyo ilikabidhiwa kwa mzee huyo wiki iliyopita na mmoja wa wahariri wa magazeti yetu, Mohammed Kuyunga, Kigogo Mbuyuni jijini Dar anakoishi. Kuyunga alisema kuwa kampuni imeguswa na hali aliyonayo Mzee Kipara hivyo kupitia simu hiyo inaamini watu wengi walioguswa na maradhi yake wataweza kumsaidia kwa hali na mali. “Hii simu tumempa pamoja na laini yenye namba 0753 92 34 54 ambayo imeunganiswa na huduma ya M-Pesa ili kuwa rahisi kwa watu kuweza kumtumia fedha,” alisema Kuyunga. N.B. Kutoa ni moyo na siyo utajiri, hivyo hima popote ulipo nchini, msaidie mzee huyu kwa kumtumia kiasi chochote utakachojaaliwa kwa njia ya M-PESA AU TIGO PESA, itamfikia mwenyewe moja kwa moja na unaweza kuongea nae kwanza. Elfu 2 utakayomtumia ina msaada mkubwa kwake na Mungu atakulipa - WEB MASTER. Global Publishers & General Enterprises Ltd P. O. Box 7534 Dar es salaam Tanzania East Africa Tel: +255 22 2773356/57, +255 22 784 888982
  • Publishers of favorite newspapers in Tanzania
  • Read: Ijumaa Wikienda & Championi Every Monday
  • Read: Uwazi Every Tuesday
  • Read: Risasi & Championi every Wednesday
  • Read: Amani every Thursday
  • Read: Ijumaa & Championi every Friday
  • Read: Risasi Every Saturday
  • You can also read them on line, Every Day, 24/7!
  • VISIT US: www.globalpublisherstz.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...