Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 12, 2014

WANNE WANYAKUA ZAWADI YA SHINDA KI-BRAZIL NA MWANASPOTI


Meneja Masoko wa Mwananchi Communications Ltd (MCL) wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen  na Mwanaspoti, Bernard Mukasa akizungumza kwa njia ya simu katika ofisi za MCL  jijini Dar es Salaam jana na mmoja wa washindi wa bahati nasibu ya Shinda Ki-Brazil ambaye ni fundi umeme, Issa Rashid Ndingo mkazi wa Kigogo aliyeshinda king’amuzi cha DSTV. Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na gazeti la Mwanaspoti. Kushoto ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo nchini, Mrisho Millao.  Pcha na Rafael Lubava


Na Mwandishi Wetu
Wasomaji wanne wa gazeti la Mwanaspoti jana Jumatano walitangazwa kuwa washindi wa kwanza wa promosheni ya Shinda Ki-Brazil na Mwanaspoti baada ya kunyakuwa zawadi mbalimbali zikiwemo vingamuzi vya Dstv pamoja na jezi.
Washindi hao wamenyakua zawadi hizo baada ya kutuma neno namba zitakazopatikana kwenye ukurasa wa tatu wa gazeti la Mwanaspoti kwenda kwenye namba 15551.Namba moja imetambulishwa kwa herufi B na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za binafsi. Namba ya pili imetambulishwa kwa herufi T na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za timu. 
Washindi wa vingamuzi vya Dstv pamoja na kifurushi kizima cha malipo kwa mwezi mmoja (Compact Plus) ni  Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla. Kwa upande mwingine aliyejishindia Jozi moja ya jezi (ina jezi 16), Jackson Fredrick wa Mwanza. 
Namenga (54) ambaye ni Afisa Mstaafu wa Jeshi na pia mkazi wa Mbagala alisema, " Nina furaha sana, nitaendelea kushiriki kwani naamini nitapata zawadi zingine."
Ndingo (42) ambaye ni mkazi wa Kigogo alisema, " Nawashukuru sana Mwanaspoti, nina uhakika wa kuona Kombe la dunia." 
Chengulla (25) ambaye ni mkazi wa Songea mjini, " Jamani someni Mwanaspoti mfaidi kama mimi, nimebahatika kwasababu nimeshiriki kwa kipindi kidogo na kushinda."
Fredrick (28) ambaye ni mwalimu alisema, " Nimefurahi kushinda jezi za kwenye promosheni hii, zawadi hii ni kwa wanafunzi wangu wa timu ya shule ya Sekondari ya Mamaye iliyopo Misungwi, Mwanza." 
Meneja Masoko wa Kampuni ya Mwananchi, Bernard Mukasa alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi zimebaki kwa wasomaji ambazo ni runinga tatu zenye ukubwa wa inchi 32, dekoda 27 za Dstv zilizounganishwa na kifurushi cha compact plus kwa muda wa mwezi mmoja, jozi tano za jezi pamoja na fedha taslim zinazotolewa kila siku mpaka shindano litakapomalizika.
Promosheni hii imeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications LTD (MCL) kupitia gazeti lake la Mwanaspoti kwa kushirikiana na kampuni ya  Multchoice Tanzania (Dstv) ikiwa na lengo la kuwaunganisha wadau wa soka nchini katika kufurahia mlolongo wote wa matukio ya michuano ya Kombe la Dunia huko Brazil.
Promosheni  hiyo ambayo ilifunguliwa rasmi  Juni 2   itafungwa Julai 12 siku ya mwisho ya mashindano hayo ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Brazil. 
xxxxxxxx

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...