Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 16, 2014

EXTRA BONGO KUPAMBA REDD'S MISS PWANI 2014



Na Happines Mnale

BENDI ya muziki wa dansi ya  Extra Bongo inayoongozwa  na mwanamuziki mkongwe nchini Camarade Ally Choki  ndiyo itakayopamba shindano la Redd’s Miss Pwani  lililopangwa kufanyika juni 27 2014 katika ukumbi wa Maisha Plus (Police Mess).

Mbali ya Choki ambaye atakuwa na kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said ‘Sharapova’ , Otilia na wengineo watanogesha na kuacha historia siku hiyo .

Hayo yalisemwa jana  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solutions (LIMSO), Khadija Kalili ambaye pia ndiyo Mratibu wa shindano hilo.

 Kalili aliongeza kwa kusema kuwa  anawaahidi wakazi wa mkoa wa Pwani na wilaya zake zote kwa jumla kupata burudani ya aina yake siku hiyo hivyo amewaomba wajitokeze kwa wingi.

Alisema katika shindano hilo warembo kumi ndiyo watakaopanda jukwaani ikiwa ni katika kumsaka malkia wa Pwani ambaye atauwakilisha Mkoa katika  shindano la kanda ya Mashariki na baadaye katika fainali za Redd’s Miss Tanzania 2014.

Kalili aliongeza kwa kusema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea  ambapo pia anawataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni wadhamini wakuu  Redd’s Premium Cold, DIRA Media Group,   Eden Herbalist Clinic ya Jijini Dar es Salaam, CXC Africa, Kitwe Traders, Michuzi Media Group, Jambo Concept, Bongoweekend.blogspot.com, Maisha Plus (Police Mess) ,  Montage (Teddzzzzz), Filbert Bayi Foundation (FBF).Kiingilio ni sh. 10,000.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...