Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 15, 2014

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA HELKOPTA KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI

Meneja Mipango na Mikakati wa Howard G. Buffet Foundation Tanzania Chapter Bi. Ellen Mutalemwa akitoa rai wakati wa hafla ya kukabidhi Helkopta moja ambayo ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mwenyekiti wa Mfuko huo alipomtembelea Rais Kikwete hivi karibuni. Helkopta hiyo imetolewa ili kusaidi juhudi za Serikali katika kupambana na ujangali katika hifadhi za Taifa
Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Helkopta kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet  (hayupo pichani) kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu.Hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiteta jambo na  Wawakilishi wa Bunge .katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa Helkopta kwa ajili kupambana na ujangili nchini Mh. James Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Maliasili na Mazingira (katikati) na Mhe. Mch. Peter Msigwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Idd Mfunda (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helkopta Charter (EA) Ltd Bw. Peter Achammer wakitiliana saini katika hati za makabidhiano ya Helkopta moja iliyotolewa kama msaada na Taasisi ya Howard G. Buffet Foundation ya nchini Marekani.Wanaoshuhudia zoezi hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu (aliyesimama kushoto) na Balozi wa Marekani hapa nchini Mark Childress

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amepanda Helkopta ambayo alikabidhiwa kama msaada kutoka Mfuko wa Howard G. Buffet kwa ajili ya kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na ujangili.

Picha na Frank Shija, WHVUM

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...