Mwakilishi
wa Kikundi cha wajasiriamali wa usafirishaji abiria kwa njia ya Bahari
cha Rehema za Mungu cha Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini “ A “
akipokea hundi ya shilingi Milioni 2,400,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi zilizotolewa na Mfuko wa
Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar..
Baadhi
ya Viongozi wa Vikundi 12 vya wajasiri amali wa Kisiwa cha Unguja
wakifuatilia hafla ya utowaji Mikopo kwa vikundi vyao kutoka mfuko wa
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya
Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto Mwanakwerekwe.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************************
Vikundi
12 vya wajasiriamali wa miradi tofauti ya Maendeleo katika Wilaya sita
za Kisiwa cha Unguja wamekabidhiwa hundi za mikopo kutoka Mfuko wa
Uwezeshaji Wananchi ulioanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mfuko
huo wenye lengo la kuwakomboa Wananchi hasa wanawake, Vijana pamoja na
wanafunzi waliomaliza mafunzo yao ya sekondari na Vyuo ulizinduliwa
rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali
Mohamed Shein Tarehe 21 mwezi Disemba mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment