Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 19, 2014

MASHINDANO YA NGALAWA YANOGESHA TAMASHA LA 17 LA ZIFF 2014 VISIWANI ZANZIBAR


DSC_0217
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya resi za Ngalawa wakijiandaa tayari kwa kuanza mashindano hayo katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF 2014 linaloendelea visiwani Zanzibar. Picha na Zainul Mzige.
**********************************************
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
NGALAWA zote 11 zilizoingia majini kukamilisha mzunguko wa saa mbili wa resi za ngalawa mjini Zanzibar zilimarisha mashamshamu hayo bila najali na timu tatu zilipewa zawadi za ushindi.
Resi za Ngalawa kama zinavyojulikana ni utamaduni halisi wa visiwa vya pemba na Unguja na ni sehemu ya tamasha kubwa la filamu la kimataifa la Zanzibar ambalo linaendelea visiwani hapa.
Kwa wale waliozaliwa maeneo ya bara, resi hizi zilikuwa kivutio kikubwa kwao kutokana na maandalizi yanayofanywa kabla ya kuingia majini na dau kunyanuliwa.
Wakati dau limenyanyuliwa, maji yamekuwa yakichotwa ama ndani ya Ngalawa au nje katika bahari kumwagia tanga katika hali inayoelezwa kuliimarisha katika ukinzani wa upepo.
“mbio za Ngalawa ni kipimo kikubwa cha Uzanzibari wetu na kila mwaka ZIFF huhitimisha utashi wake wa kuwa na tamasha la nchi za jahazi kwa kuwa na mbio za ngalawa” alisema mshehereshaji Muslim Nassoro Abdalla katika shamrashamra zilizofanyika ufukweni kandoani mwa hoteli ya Tembo.
DSC_0235
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (mwenye t-shirt ya njano) akupiliza Kipenga kuashiria kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye fukwe za Hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.
Muslim ambaye alisema kwamba mwaka huu walitaka kuwa na mbio za timu 20 (ngalawa) walishindwa kuhitimisha ndoto hiyo kutokana na masuala nje ya uwezo wa ZIFF.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...