Oxfam wafanya Ziara ya Mafunzo Bagamoyo na Kuzindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kuongoza mjadala wa hali halisi ya kilimo na
uzalishaji wa chakula Bagamoyo uliofanyika kijiji cha Zinga, Bagamoyo
hivi karibuni. Mjadala huu uliratibiwa na Oxfam na kuwahusisha
wakulima wanawake kama mpango endelevu wa Oxfam kutambua na kuthamini
mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa chakula.
Meneja
Kampeni wa Oxfam, David Moriarty (kulia), akigawa fomu za kushiriki
shindano la 'Mama Shujaa wa Chakula' kwa kina mama wa kijiji cha Zinga
wilaya ya Bagamoyo hivi karibuni mara baada ya kuzindua shindano hilo.
Shindano la 'Mama Shujaa wa Chakula' linaratibiwa na Oxfam kutambuwa
na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji wa
chakula.
Mkulima
kutoka kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo, Halima Mwinshehe akitoa
hoja yake wakati wa mhadhara ulioandaliwa na Oxfam kuzungumzia kilimo
na maswala ya lishe uliofanyika kijini hapo mkoani Pwani hivi
karibuni. Mhadhara huu ni moja ya mpango endelevu unaoratibiwa na
Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye
uzalishaji wa chakula.
Mkulima
na mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula kutoka Nigeria,
Briskila Jerome akiwahamasisha akina mama wenzake wa kijiji cha Zinga
wilaya ya Bagamoyo hivi karibuni, kujiunga na shindano la 'Mama Shujaa
wa Chakula' kwa upande wa Tanzania. Shindano hili linaratibiwa na Oxfam
kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima kwenye uzalishaji
wa chakula.
Wakulima
wanawake na wataalamu wa chakula kutoka Oxfam wakiangalia zao la
muhogo, wakati walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wanawake
katika kijiji cha Zinga wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani hivi karibuni.
Wataalamu hawa wa chakula walikuwa nchini kwenye ziara ya mafunzo
katika maswala ya lishe na mchango wa wakulima wanawake kwenye
uzalishaji wa chakula.
Wakulima
wanawake kutoka vikundi mbalimbali katika kijiji cha Zinga wilaya ya
Bagamoyo wakipata futari baada ya kumalizika kwa mjadala wa hali
halisi ya kilimo na uzalishaji wa chakula wilayani humo. Mjadala huu
uliratibiwa na Oxfam na kuwahusisha wakulima wanawake kama mpango
endelevu wa Oxfam kutambua na kuthamini mchango wa wanawake wakulima
kwenye uzalishaji wa chakula.
No comments:
Post a Comment