Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 30, 2012

GAZETI LA Mwana Halisi LAFUNGIWA


SERIKALI ya Jamhuri ya Tanzania, imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwakile kilichoelezwa kuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchozezi.
Sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi. 
Akisoma tamko la Serikali leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
“Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii,pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari”alisema
Aidha alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
“Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulika kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i),adhabu hiyo itaanza tarehe 30 julai,2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dra es salaam julai 27,2012”alisema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...