Eden Hazard
LONDON, England
“Messi ni Mchezaji Bora wa Dunia na nisenme wazi kwamba matarajio yangu ni kuwa mzuri kama yeye na naamini nitaweza”
YOSO mpya klabuni Staaamford Bridge, Eden
Hazard, amepanga kufanya vitu vikubwa katika Ligi Kuu ya England na
kusema atahakikisha anakuwa Lionel Messi wa ligi huyo pendwa duniani kwa
sasa.
Mkali huyo mwenye miaka 21 raia wa
Ubelgiji, ametua Darajani kwa dau nono la puani milioni 32 akitokea
Lille ya Ufaransa na sasa anapania kujiweka juu sawa na thamani yake.
Nyota huyo hufurahi zaidi anapofananishwa
na Messi Mchezaji Bora wa Dunia na shujaa wa FC Barcelona, ambapo
alikataa ofa za kujiunga na klabu kubwa duniani ili kutimiza ndoto za
kuchezea Blues.
Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu
kukamilisha uhamisho wake kutoka Ligue 1 na kutua Ligi Kuu, Hazard
aliiambia SunSport: “Messi ni Mchezaji Bora wa Dunia na nisenme wazi
kwamba matarajio yangu ni kuwa mzuri kama yeye na naamini naweza.
“Lakini nina furaha kubwa watu wanapofanya
ulinganisho baina yetu na kunifananisha na Messi kunaniongezea ujasiri
na kutafakari nia zitakazoniwezesha kupata mafanikio nikiwa Chelsea
badala ya kuwaza vikwazo katika kunifikisha huko.
“Hatimaye kocha anabaki kuwa mtu wa mwisho
kuamua kunichezesha mimi katika nafasi ambayo Messi anacheza akiwa
Barca, lakini binafsi naangalia namna itakayonipa madfanikio kupitia
njia nayopaswa kupitia.”
Mchezaji Bora Bora huyo wa zamani wa
Ufaransa, alikataa ofa za kujiunga Manchester City na Manchester United
kiangazi na kukubali dau la mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki akiwa na
jezi za Bluu za Chelsea, ambao ni mabingwa wa soka barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment